Leo Kombe la RPC ndani ya Manispaa ya Lindi imeendelea kwa kuzikutanisha Timu Nne kutoka katika makundi ya A na B, ambapo kundi A zilikutana timu za Kata ya Mingoyo na Chikonji Pia Kundi B Tandangongoro na Rasibula.
Katika Mchezo wa Kwanza uliozihusisha timu za Kundi B, Tandangongoro walikubali kichapo cha magoli 2-1 kutoka kwa Rasibula, ambapo mchezo huo ulikuwa wa kuvutia kwani Tandangongoro walionyesha kandanda safi japo walipoteza point tatu katika mchezo huo. Goli la kwanza lilifungwa mnamo dakika ya 34 kupitia kwa Lokorence James na goli hilo kudumu hadi kipindi cha kwanza kinamalizika.
Kipindi cha pili Kilianza kwa Tandangongoro kulisakama lango la wapinzani wao na halihiyo ilizaa matunda mnamo dakika ya 74 ya mchezo kupitia kwa Idrisa mtivila aliweza kuisawazishia timu yake goli lakini goli hilo halikuweza kudumu kwani Msafiri Kambwili aliweza kuizimisha furaha yao kwa kuipatia timu yake ya Rasibura Goli la Pili na la ushindi mnamo dakika ya 84.
Hadi Mwisho wa Mchezo huo Matokeo yalibakia Tandangongoro 1 - Rasibula 2.
Kipute cha Pili kilianza majira ya saa Kumi kamili za jioni zikikutanisha Timu za kata ya Mingoyo na Chikonji na Katika Mchezo huo Timu ya Kata ya Mingoyo ilionyesha kiwango kizuri na kuweza kutawala mchezo huo na waliweza kuwaadhibu wapinzani wao kwa jumla ya magoli 3-0. Magoli hayo yalifungwa na Najim Issa mnamo dakika ya 3, Hamisi Matongodi dakika ya 46 na Salum mohamed Dakika ya 55.
Kesho Ligi hiyo itaendelea kwa kuzikutanisha Timu za kata ya KITUMBIKWELA Vs MTANDI ambayo mechi hiyo itaanza majira ya saa nane kamili mchana Mechi ya Pili ni kati ya MAKONDE Vs MIKUMBI.
Kipindi cha pili Kilianza kwa Tandangongoro kulisakama lango la wapinzani wao na halihiyo ilizaa matunda mnamo dakika ya 74 ya mchezo kupitia kwa Idrisa mtivila aliweza kuisawazishia timu yake goli lakini goli hilo halikuweza kudumu kwani Msafiri Kambwili aliweza kuizimisha furaha yao kwa kuipatia timu yake ya Rasibura Goli la Pili na la ushindi mnamo dakika ya 84.
Kikosi cha Kwanza cha Timu ya Kata ya Tandangongoro kilichocheza dhidi ya Timu Kata ya Mingoyo
Kikosi cha Kwanza cha Timu ya Kata ya Mingoyo kilichocheza dhidi ya Timu Kata ya Tandangongoro
Nice one...
ReplyDelete