Halmashauri ya Mtama, Wilaya ya Lindi, imejipanga kikamilifu katika maandalizi ya mapokezi ya Mwenge wa Uhuru 2025, ambapo maandalizi ya mbio hizo yameanza mapema ili kuhakikisha uratibu na utekelezaji wake unafanikiwa.
Mwenge wa Uhuru utapokelewa kimkoa katika Mkoa wa Lindi tarehe 26 Mei 2025, Kata ya Sudi, katika Kijiji cha Madangwa na kisha kusafirishwa kuelekea Halmashauri ya Mtama.
Katika Halmashauri ya Mtama, Mwenge wa Uhuru utatembelea shughuli mbalimbali. Kauli mbiu ya mwaka huu ni: "Jitokeze Kushiriki Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kwa Amani na Utulivu", ikilenga kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi huo, huku wakizingatia amani na utulivu.
Maandalizi ya mapokezi ya Mwenge wa Uhuru 2025 katika Halmashauri ya Mtama yanaendelea kwa kasi, na viongozi wa eneo hilo wanasisitiza kuwa kila jambo linapaswa kuwa tayari ili kuhakikisha mbio hizo za Mwenge wa Uhuru zinatekelezwa kwa mafanikio.