VIWANJA VINNE VYAFUNGIWA NA TFF

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza kufunga viwanja vya Jamhuri, Dodoma, CCM Kirumba, Mwanza, na Liti, Singida kutumika kwa michezo ya Ligi kutokana na kushindwa kukidhi vigezo vya kikanuni na sheria za mpira wa miguu.

Miundombinu ya viwanja hivyo haikufikia viwango vinavyotakiwa kulingana na Kanuni ya Leseni za Klabu.

Kwa uamuzi huu, timu zinazocheza michezo yao ya nyumbani katika viwanja hivyo zitahitajika kutumia viwanja vingine kama ilivyoainishwa katika Kanuni, hadi viwanja hivyo vitakapofanyiwa marekebisho na kukaguliwa na TFF.

TFF imezitaka klabu zote kuendelea kutunza na kuboresha miundombinu ya viwanja ili kuepuka usumbufu kama huu katika siku zijazo.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post