HATUTACHEZA TENA NA SIMBA MSIMU HUU

Baada ya Yanga Sc kukamilisha taratibu zote kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Simba, ambao ulipaswa kufanyika jana saa 1:15 usiku katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Klabu ya Yanga imeweka msimamo wa kutocheza tena mchezo mwingine dhidi ya Simba katika ligi msimu huu. Hii ni baada ya bodi ya ligi kuahirisha mchezo huo bila kutoa sababu za msingi.

Andiko la Makamu wa Rais wa Yanga, Arafat Haji, limeweka tamko rasmi na kufunga mjadala kuhusu msimamo wa klabu. Yanga imesisitiza kuwa mchezo wa Derby kati yao na Simba ulimalizika rasmi tarehe 08 Machi, na sasa wanazingatia ratiba nyingine za ligi. Klabu hiyo haitakuwa tayari kurudishwa nyuma kwa ajili ya mechi nyingine dhidi ya Simba msimu huu.

Makamu huyo wa Rais wa Yanga ameandika Hivi:-

"WANANCHI, mechi yetu dhidi ya Mtani wetu SIMBA imeisha leo hii kwa msimu wa 2024/25 raundi ya pili na ieleweke vyema hakutakuwa na mechi nyingine sehemu nyingine, siku nyingine na tarehe nyingine yoyote ya kuihusu Yanga dhidi ya Simba kwa Ligi kuu, iwekwe sawa kwenye kumbukumbu na ikolezwe vyema kwa wino kuwa its done and dusted, sisi tunasonga mbele na ratiba zingine.

Hii ndio sauti yenu moja, kamba moja ya DAIMA MBELE, NYUMA MWIKO na tutashikilia hapo hapo Wananchi, niwatakie safari njema Wananchi wote kurejea makwenu, Mungu awalinde, awatunze mkaungane tena na familia zenu, tutakutana tena wakati mwingine panapo majaaliwa In shaa Allah".

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post