Unknown Unknown Author
Title: MWANAMKE WA KITANZANIA AKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA AINA YA COCAINE NCHINI INDIA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Thelma Mkandawire (38) raia wa Zambia na Pamela Devid Kiritta (41) raia wa Tanzania baada ya kukamatwa na kilo nne za cocaine leo nchini...
Thelma Mkandawire na Pamela Devid Kiritta
Thelma Mkandawire (38) raia wa Zambia na Pamela Devid Kiritta (41) raia wa Tanzania baada ya kukamatwa na kilo nne za cocaine leo nchini India.

Wanawake wawili wamekamatwa leo Jumamosi na kilo nne za cocaine nchini India. Wanawake hao wametajwa kama Pamela Devid Kiritta mwenye umri wa miaka 41 raia wa Tanzania na Thelma Mkandawire mwenye umri wa miaka 38 raia wa Zambia.

Wanawake hao wamekamatwa ndani ya hoteli moja iliyoko kusini mwa jiji la New Deilhi baada ya maafisa husika kutonywa kuwa walikuwa wanapeleka mzigo huo wa cocaine kwa mtu fulani. Mwanamke wa Zambia alisafiri na ndege ya kampuni moja ya Ulaya akitokea Addis Ababa. Maafisa hao walianza kumfuatilia mara tuu alipotua kwenye uwanja wa kimataifa wa ndege wa IGI.

Baada ya kucheki out, Mzambia huyo alichukua teksi na kuondoka zake. Maafisa walimfuatilia mpaka kwenye hoteli moja iliyopo eneo la Mahipalpur ambapo partner wake Pamela alikuwa anasubiria mzigo. Wote wawili walikamatwa kabla ya kuondoka hotelini hapo. Ndani ya begi la Mzambia kulikuwa na mzigo wa kilo nne za cocaine ambazo zilikuwa zimefungwa kwa ustadi mkubwa sana kiasi kwamba machine za airport hazikuweza kugundua.

Alipohojiwa na maafisa hao, Pamela alisema alikuwa amepanga kwenye flat moja iliyoko Vasant Kunj tokea Januari 20 mwaka huu. Pamela amesema kuwa alikuwa anamfanyia kazi mwanaume mmoja wa Afrika ya Kusini.


Pamela ameitembelea India mara tisa tokea mwaka 2006. Pia Pamela ameshatembelea nchini nyingine kama Ecuador, Afrika Ya Kusini na Kenya. Maafisa wa India wanahisi kuwa safari zake zinahusiana na biashara ya dawa za kulevya.

Kwa upande wa Mzambia (Thelma) alikamatwa Pakistani mwaka 2015 kwa tuhuma za kusafirisha dawa za kulevya. Pia ametemblea nchi za China na Hong Kong kwa biashara hiyo hiyo.
Source: JamiiForums
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
KUWA KARIBU NASI LINDIYETU.COM
Usipitwe!! Ungana na Familia hii kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata Infortainment zote!! Usikose kujiunga na Youtube channel yetu ili kupata Exclusive mbalimbali kali kutoka LindiYetu TV

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top