BEKI WA YANGA IBRAHIM BACCA APANDISHWA CHEO

Beki wa klabu ya Yanga SC, Ibrahim Hamad 'Bacca', amepandishwa cheo na Kikosi Maalumu cha Kuzuia Magendo Zanzibar (KMKM) kutoka kuwa Koplo hadi Sajenti, kutokana na utendaji wake bora katika mchezo wa soka.

Akizungumza baada ya uteuzi wake, Sajenti Ibrahim 'Bacca' alieleza furaha yake kwa kupewa nafasi hiyo, akisema, “Nashukuru kwa msaada wa kikosi changu cha KMKM, ambao walinisaidia kila hatua. Nitaendelea kujitolea kwa ajili ya nchi yangu na kazi yangu ya soka.”

KMKM, ambacho ni kikosi cha ulinzi cha Zanzibar, kinajukumu la kulinda mipaka ya bahari dhidi ya magendo, uvuvi haramu, na vitendo vingine vya kihalifu. Pia, hufanya kazi muhimu za uokoaji baharini na kuhakikisha usalama wa majini.

Hata hivyo, licha ya kazi yake ya kijeshi, Bacca ameendelea kuwa sehemu ya Yanga SC na kudhihirisha ushirikiano mzuri kati ya michezo na ulinzi.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post