Desemba 23 miaka 63 iliyopita mkuu wa zamani wa shirika la kuogofya la usalama na la siri la Urusi ya zamani ambaye pia alikuwa kiongozi nambari mbili wa nchi hiyo katika zama za Joseph Stalin, Lavrenty Pavlovicha Beria, alihukumiwa kifo na kunyongwa kwa tuhuma za kwenda kinyume na misingi ya sheria za Chama cha Kikomonisti sambamba na kufanya njama dhidi ya serikali.
Katika kipindi cha utawala wa Stalin, Pavlovicha Beria alitoa amri ya kuuawa watu wengi na akafanya umwagaji damu ndani ya Chama cha Kikomonisti na katika Jeshi Jekundu la Urusi ya zamani.
Siku kama ya leo miaka 68 iliyopita watu saba miongoni mwa viongozi mashuhuri wa Japan wakati wa Vita vya Pili vya Dunia walinyongwa, kufuatia hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Tokyo. Mahakama hiyo ambayo iliundwa ikiwa ni katika muendelezo wa mahakama ya Nuremberg ya Ujerumani ili kuwahukumu watenda jinai za kivita huko Japan, iliwahukumu viongozi 25 wa Japan ambapo 18 kati yao walihukumiwa kwenda jela.
Waziri Mkuu wa wakati huo wa Japan, Hideki Tojo alikuwa kiongozi wa ngazi za juu zaidi aliyefikishwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Tokyo na kuhukumiwa adhabu ya kunyongwa.
Na siku kama ya leo miaka 28 iliyopita alifariki dunia mwanazuoni mkubwa wa Kiislamu Allamah Mirza Jawad Agha Tehrani. Alipata elimu ya msingi mjini Tehran na baadaye alielekea katika miji mitakatifu ya Qum na Najaf, Iraq kwa ajili ya elimu ya juu.
Allamah Agha Tehrani alikwea kwa kasi daraja za elimu na kuwa miongoni mwa wanazuoni wakubwa. Alisifika sana kwa uchamungu, zuhudi na kuwapenda sana Watu wa Nyumba ya Mtume Muhammad (saw). Miongoni mwa vitabu vya msomi huyo mkubwa wa Kiislamu ni Aine Zendegi na Mizanul Matwalib.
_________________________________________
- ULIPITWA NA HII YA QEENDARLEEN KUMTOSA ALIKIBA?
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.