Katika Muendelezo wa Mechi za ligi ya Kombe la RPC Manispaa ya Lindi imeendelea leo na kuzikutanisha Timu za Kata ya Nachingwea na Msinjahili ambapo timu hizo zipo katika Kundi A na Rahaleo Vs Mtanda B kutoka Kundi B.
Katika Mchezo wa kwanza uliochezwa majira ya Saa nane Mchana ndani ya uwanja wa Ilulu Timu hizo zilitoshana nguvu. Hadi kipyenga cha Mwisho matokeo yalikuwa Nachingwea 0 - Msinjahili 0.
Saa Kumi ulichezwa mchezo wa Kundi B ambapo Timu za Kata ya Rahaleo na Mtanda B zilikutana na Rahaleo ndio walioibuka kidedea baada ya Mpambano huo Mkali ambao ulikuwa burudani kwa watazamaji kwa Kuonesha Kandanda safi kabisa.
Ni Abou Kipara ndie alikuwa wa kwanza kuziona nyavu za Mtanda B kwa kufunga bao safi kabisa dakika ya 19 baada ya kuwachambua mabeki pamoja na Golikipa na kuusukumia mpira wavuni posipokuwa na tatizo lolote. Iliwachukua dakika 29 tu kuongeza Goli la pili kupitia kwa Mchezaji wao Issa Hamisi mnamo dakika ya 40 ya mchezo.
Mtanda B walionekana kujipanga zaidi baada ya Kocha wao kufanya Marekebisho katika safu ya Ushambuliaji na kuweza kupata matunda ya Marekebisho hayo kwani Yusuph Hamisi aliweza kuipatia Timu yake goli la kufutia machozi mnamo dakika ya 45 ya Kipindi hicho cha Kwanza.
Hadi Mpira unamalizika Matokeo yalibakia kuwa Rahaleo 2 - Mtanda B 1.
Kesho ligi hiyo itaendelea kwa Kuzikutanisha Timu za Kundi B ambazo ni Tandangongoro Vs Rasibula ambayo mechi hii itachezwa saa nane kamili Mchana. Na mechi ya Pili ni kutoka Kundi A ambazo ni Mingoyo Vs Chikonji.
Saa Kumi ulichezwa mchezo wa Kundi B ambapo Timu za Kata ya Rahaleo na Mtanda B zilikutana na Rahaleo ndio walioibuka kidedea baada ya Mpambano huo Mkali ambao ulikuwa burudani kwa watazamaji kwa Kuonesha Kandanda safi kabisa.
Mtanda B walionekana kujipanga zaidi baada ya Kocha wao kufanya Marekebisho katika safu ya Ushambuliaji na kuweza kupata matunda ya Marekebisho hayo kwani Yusuph Hamisi aliweza kuipatia Timu yake goli la kufutia machozi mnamo dakika ya 45 ya Kipindi hicho cha Kwanza.
Kikosi cha Kwanza cha Timu ya Kata ya Mtanda B kilichocheza dhidi ya Timu ya Kata ya Rahaleo zote za Manispaa ya Lindi
Kikosi cha Kwanza cha Timu ya Kata ya Rahaleo kilichocheza dhidi ya Timu ya Kata ya Mtanda B zote za Manispaa ya Lindi.
Kesho ligi hiyo itaendelea kwa Kuzikutanisha Timu za Kundi B ambazo ni Tandangongoro Vs Rasibula ambayo mechi hii itachezwa saa nane kamili Mchana. Na mechi ya Pili ni kutoka Kundi A ambazo ni Mingoyo Vs Chikonji.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.