Waziri wa Fedha Mhe. Dkt.
Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiwasilisha bungeni jijini Dodoma,
Mapendekezo ya Mfumo na Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2025/2026
kwenye Kamati ya Bunge zima, bungeni jijini
Dodoma.
Waziri wa Fedha Mhe. Dkt.
Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiteta jambo na Katibu Mkuu Wizara ya
Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, baada ya kuwasilisha Mapendekezo ya
Mfumo na Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2025/2026 kwenye Kamati
ya Bunge zima, bungeni jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha Mhe. Dkt.
Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (wa tatu kushoto mstari wa mbele) na Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, (wa
tatu kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi waandamizi wa
Wizara ya Fedha, Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, na Tume ya Mipango,
baada ya kuwasilisha Mapendekezo ya Mfumo na Ukomo wa Bajeti ya
Serikali kwa Mwaka 2025/2026 kwenye Kamati ya Bunge zima, bungeni jijini
Dodoma.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt.
Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amewasilisha Mapendekezo ya Mfumo na Ukomo
wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2025/26, kwenye Kamati ya
Bunge zima, katika Ukumbi wa Pius Msekwa, Bungeni jijini Dodoma, ambapo
Serikali imependekeza kukusanya na kutumia jumla ya shilingi trilioni
57.04 kwa mwaka 2025/26, sawa na ongezeko la asilimia 13.4
ikilinganishwa na Bajeti ya Mwaka wa Fedha, 2024/25 ya shilingi trilioni
50.29.
Hafla
hiyo imeongozwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.
Kassim Majaliwa na kuhudhuriwa pia na Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Mussa
Azan Zungu, na viongozi waandamizi wa Serikali.
Tags
HABARI ZA KITAIFA