Unknown Unknown Author
Title: NGASSA, MRWANDA NA TAMBWE WAIONGOZA YANGA SAFU YA USHAMBULIAJI, TELELA BENCHI LEO DHIDI YA BDF XI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
TAMBWE, MSUVA NA NGASA WAKISHANGILIA GOLI KWA PAMOJA, (PICHA NA MAKTABA) Na Iblahim Karim,Dar es Salaam. KOCHA Mholanzi Hans Van Pluijm...
Yanga SC
TAMBWE, MSUVA NA NGASA WAKISHANGILIA GOLI KWA PAMOJA, (PICHA NA MAKTABA)

Na Iblahim Karim,Dar es Salaam.
KOCHA Mholanzi Hans Van Pluijm amewaanzisha kwa pamoja Mrisho Ngassa,Amisi Tambwe,Simon Msuva na Danny Mrwanda katika safu ya Ushambuliaji dhidi ya BDF XI leo.

Yanga SC itamenyana na BDF XI leo Saa 1:00 Usiku kwa saa za huko na saa 2;00 kwa saa za Afrika Mashariki katika mchezo wa marudiano,Raundi ya Awali kombe la Shirikisho Afrika na Mholanzi huyo amepanga washambuliaji wenye kasi.

Tambwe hana kasi kulinganisha na Msuva,Mrwanda na Ngassa lakini ni mpiganaji pale mbele na anauwezo mmkubwa wa kufunga.

Tambwe ndiye aliyefunga mabao yote mawili katika mchezo wa Awali wiki iliyopita.
Mrwanda ameingia kwenye kikosi cha kwanza kuchukua nafasi ya Mbrazil Andrey Countinho ambaye ameachwa Dar es Salaam kwa sababu ya majeruhi.

Safu ya kiungo ya Yanga leo itaundwa Mbuyu Twite chini na juu Haruna niyonzima maana yake kiungo ammbaye amekuwa akicheza vizuri siku za karibuni Salum Telela 'Master' anakosekana.

Hakuna mabadiliko kwenye safu ya Ulinzi Ally Mustapha akianza langoni,kulia Juma Abdul kushoto Oscar Joshua katikati Kevin Yondani na Nahodha Nadir Haroub 'Canavarro'

Kikosi kamili;
Ally Barthez,Juma Abdul,Oscar Joshua,Kevin Yondani,Nadir Haroub,Mbuyu Twite,Haruna Niyonzima,Amisi Tambwe,Danny Mrwanda Mrisho Ngassa

Katika Benchi;
Deo Munishi 'Dida', Said Juma 'Kizota' Hussein Javu, Kpah Sherman, Hassan Dilunga, Salum Telela na Rajab Zahir.

Azam tv inatarajiwa kuonyesha moja kwa moja mchezo huo kutoka Uwanja wa Lobetse Saa 2;00 Usiku.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top