Maafisa Hesabu Wakuu, Kitengo cha Huduma za Mfuko Mkuu (CFS), Wizara ya Fedha, Bi. Joyce Chacky na Bi. Mercelina Haule, wakitoa elimu kwa wananchi waliotembelea Banda la Wizara ya Fedha, katika Maadhimisho ya Kimataifa ya Siku ya Wanawake Duniani, yanayofanyika katika Uwanja wa Sheikh Amiri Abeid, jijini Arusha.
.jpg)
Na. Mwandishi Wetu, Arusha
Wizara ya Fedha imeungana na washiriki wengine kutoa elimu kwa umma kuelekea maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, ambayo yatafanyika kitaifa jijini Arusha. Maadhimisho haya, yanayotarajiwa kufikia kilele siku ya tarehe 8 Machi, 2025, yatahudhuriwa na mgeni rasmi, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni "Wanawake na Wasichana 2025: Tuimarishe Haki, Usawa na Uwezeshaji." Lengo kuu la maonesho haya ni kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kuimarisha haki, usawa, na uwezo wa wanawake na wasichana katika nyanja mbalimbali, ikiwemo uchumi, elimu, na siasa.
Wizara ya Fedha, kwa kushirikiana na wadau wengine, itahakikisha kuwa umma unapata elimu kuhusu jinsi ya kushiriki kikamilifu katika juhudi za kuhakikisha wanawake na wasichana wanapata haki zao za msingi na fursa za kujitegemea katika jamii.