NDEGE YA JWTZ YAPATA AJALI JIJINI MWANZA LEO

Ajali ya Ndege Mwanza
Ndegevita moja ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ikiteketea kwa moto huku jitihada za kuuzima zikiendelea katika ajali iliyotokea leo Februari 27, 2015 katika uwanja wa ndege wa kijeshi wa Mwanza
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linapenda kutoa taarifa ya ajali ya Ndegevita moja (1) iliyotokea leo tarehe 27 Februari 2015 katika uwanja wa ndege wa kijeshi wa Mwanza.

Ndegevita za JWTZ zilikuwa katika mazoezi ya kawaida ya kivita,  Wakati rubani wa ndegevita iliyopata ajali akijiandaa kuruka ndipo ndege mnyama akaingia katika moja ya injini zake na kusababisha ndegevita kuwaka moto. 

Hata hivyo, rubani wa ndegevita hiyo Meja Peter Lyamunda  alipoona ndege yake inawaka moto alifanikiwa kujirusha nje ya ndege hiyo kwa kutumia vifaa maalum na kufanikiwa kuokoa maisha yake ingawa amepata majeraha katika mguu wakati wa kujiokoa. Kwa sasa hali yake ni nzuri anaendelea na matibabu ya kawaida .

Wananchi wasiwe na hofu hii ni ajali ya kawaida , waendelee na shughuli kama kawaida na kwamba sehemu ilipoangukia haikuleta madhara yoyote ya binadamu, nyumba wala miundo mbinu. 

Ajali ya Ndege Mwanza 
Ajali ya Ndege Mwanza
Baadhi ya Maafisa wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiwa eneo la tukio kuangalia mabaki ya ndegevita hiyo iliyopata ajali leo.
Ajali ya Ndege Mwanza
Ajali ya Ndege Mwanza
Ajali ya Ndege Mwanza

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post