Unknown Unknown Author
Title: MARKET PLACE YAINYUKA TIMBALAND FC KUTOKA NACHINGWEA 2 - 0. FAINALI YA KWANZA LIGI DARAJA LA TATU
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Benchi la Ufundi la Timu ya Market Fc leo hii ndani ya Uwanja wa Ilulu katika mchezo wa Ligi daraja la tatu ngazi ya Mkoa dhidi ya Timba...
Market Place Fc Vs Timbaland Fc
Benchi la Ufundi la Timu ya Market Fc leo hii ndani ya Uwanja wa Ilulu katika mchezo wa Ligi daraja la tatu ngazi ya Mkoa dhidi ya Timbaland fc ya Nachingea, Marketi Place Fc ilishinda 2 - 0 
Market Place Fc Vs Timbaland Fc
Benchi la Ufundi la Timu ya Timbaland Fc leo hii ndani ya Uwanja wa Ilulu katika mchezo wa Ligi daraja la tatu ngazi ya Mkoa dhidi ya Marketi Place Fc ya Lindi Mjini, Marketi Place Fc ilishinda 2 - 0 

Na.Mwandishi Wetu, Lindi
Leo katika Uwanja wa Ilulu timu ya Marketi Place Ilikuwa Mwenyeji wa Mchezo wa Fainali ya Kwanza ya Ligi daraja la Tatu ngazi ya Mkoa wakiikaribisha timu ya Nachingwea Timbaland ambayo imerudi nyumbani kwao kwa kichapo cha Bao 2 - 0.

Mchezo huo ulikuwa wa ainayake kama ilivyo kwa mechi zilizopita zilionesha ushindani mkubwa kutokana na timu zote mbili kuwa na uchu wa ushindi lakini Bahati haikuwa upande wa Timu ya Timbaland Fc Hivi leo kwani Mnamo dakika ya Nyongeza ya Kipindi cha Kwanza Timu ya Marketi Place iliweza kujipatia Goli la Kuongoza kupitia kwa Mchezaji wake Mohamed Mtaa.

Kipindi cha Pili kilianza kwa timu ya Timbaland Fc kupeleka mashambulizi ya hapa na pale langoni mwa Timu pinzani lakini mabeki walikuwa makini na kuweza kuondo hatari hizo langoni mwao.

Dakika ya 79 ya Mchezo huo Mchezaji yule yule Mohamed Mtaa aliweza kuipatia Timu yake hiyo ya Market place a.k.a wazee wa Best Loser goli la Pili.

Hadi mwisho wa Mchezo huo Matokeo yalibaki kuwa Market Place 2 - Timbaland Fc 0

Katika Hali iliyowashtua mashabiki waliojitokeza kwa wingi kutazama mchezo huo siku ya leo ni pale waamuzi walipogomea mchezo huo kuendelea kipindi cha pili kwa kukosekana kwa Vyombo vya Ulinzi na Usalama ndani ya uwanja huo, Hivyo kufanya mchezo huo kuchelewa kuanza katika kipindi cha pili.

Fainali ya Pili inatarajiwa kuchezwa siku ya Jumatano Mjini Nachingwea.

Market Place Fc Vs Timbaland Fc
Wachezaji wa Market Place wakishangilia Goli la kwanza lilifungwa na Mohamed Mtaa dhidi ya Timbaland Fc dakika ya 45 ya Kipindi cha kwanza
Market Place Fc Vs Timbaland Fc
Refa wa Mchezo wa leo wa Ligi daraja la Tatu ngazi ya Mkoa kati ya Market Place Fc (Lindi) na Timbaland Fc (Nachingwea) akiteta jambo na Makapteini kabla ya kuanza kipindi cha pili cha mchezo huo. Marketi Place Fc ilishinda mchezo huo kwa 2 - 0. 
Market Place Fc Vs Timbaland Fc
Hakika ilikuwa siku nzuri kwao Marketi Place Fc kwani waliweza kupata goli la pili la kuongonza na walishangilia vilivyo ushindi huo. Goli lilifungwa na Mohamed Mtaa kwa mara nyingine. 
Market Place Fc Vs Timbaland Fc
Kocha wa Timbaland Fc akijaribu kutoa maelekezo kwa Mchezaji wake hii ni Baada ya kuwa nyuma kwa Goli 2 - 0.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top