Ni bata kwenda, bata kufika na bata kurudi ambapo Watanzania waliovutiwa kujiunga nasi kwa pamoja tunaenjoy kwenye miaka 13 ya kuzaliwa kwa CLOUDS FM lakini pia kusherehekea ujio wa kamanda mpya wa 88.5 Dar es salaam baada ya kumaliza mkataba wa 88.4 kwa kipindi cha miaka 13.
Safari itaanza asubuhi december 28 2012 saa mbili kamili pale TAZARA na tutatumia saa nne njiani tukiwa kwenye treni huku tukipita kwenye vivutio mbalimbali vya Tanzania kama mbuga ya wanyama ya Seluu na kwenye chemchem inayotoa maji ya moto.
Kwenye treni kutakua na huduma ya chakula na vinywaji ambavyo vitakua vinatembezwa na kigari maalum ndani ya treni, mtu yeyote akiwa kwenye behewa lolote anaweza kutembea na kuingia kwenye behewa jingine, vilevile kuna madaktari wameandaliwa kuhusika na huduma ya kwanza iwapo itahitajika, pia pamoja na mambo mengine kuna behewa special ambalo limetengwa kwa watu kupumzika.
Jingine.
