Unknown Unknown Author
Title: LIGI DARAJA LA TATU NGAZI YA MKOA YAANZA KUTIMUA VUMBI UWANJA WA ILULU
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Ligi daraja La tatau ngazi ya Mkoa wa Lindi imeendelea katika hatua ya pii hapo jana na kuzikutanisha Jumla ya timu nne ambazo zinatoka sehe...

DSC07054Ligi daraja La tatau ngazi ya Mkoa wa Lindi imeendelea katika hatua ya pii hapo jana na kuzikutanisha Jumla ya timu nne ambazo zinatoka sehemu za Kilwa, Lindi na Ruangwa..

Mechi za Fungua Dimba ilikuwa Kati ya Kusini Soccer (Lindi mjini) Vs Cap Town FC (Ruangwa) ambayo ilichezwa kuanzia majila ya saa kumi na nusu saa za Afrika mashariki

Ni Timu ya Kusini Soccer Ndio ilikuwa ya kwanza kufungua ukurasa wa magoli katika ligi hiyo kupitia mchezaji wao Machachari Msafiri Kambwili baada ya kupokea Cros nzuri na kumkuta na yeye bila ajizi akaweka wavuni. hadi kipindi cha kwanza kinaisha Matokeo yalikuwa Kusini Soccer 1 – 0 Captown Fc.

DSC07057Kipindi Cha pili kilianza kwa Kasi na kufanya walinzi wa Timu ya Captown kukosa maarifa na kuruhusu mashambulizi ya hapa na pale na kufanikisha Goli la pili kupitia Mshambuliaji yule yule Msafiri Kambwili.

Mpira ulizidi kupendeza kwa mashabiki wa Kusini soccer mara baada ya kupata magoli mawili kwani walizidi kutawala mchezo huo na kuweza kufika langoni mwa wapinzani wao mara kadhaa…Kocha alifanya marekebisho kwenye safu ya ushambuliaji kwa timu ya Kusini Soccer kwa Kumtoa Msafiri Kambwili na Kumuingiza Muksini Rashidi ambaye pia alionekana mwiba kwa Mabeki wa Captown Fc ambao walikuwa wamesha choka.

Muksini Rashidi ilimchukua dakika 10 tu tangu alipoingia kuandika Bao la tatu dakika ya 64 ya mchezo na kufanya matokeo hayo kuwa 3 – 0. dakika ya 67 huyo huyo Muksini rashidi alipeleka majonzi tena kwa mashabiki na wapenzi wa Captown kwa Kufunga bao la nne na kufanya mchezo huo kuisha kwa matokeo ya 4 – 0.

KARIAKOO FC V/s KILWA STARSDSC07065Leo hii Ligi hiyo Imeendelea kwa Kuzikotanisha timu za Kariakoo Fc Vs Kilwa Stars na ni Kariakoo Fc ndio waliweza kuibuka kidedea katika mechi hiyo iliyojaa vioja kwa mashibiki wake kwani walinong’ona kuwa shirki ilikuwa imeongoza katika timu hizo kwani mipira iliyopigwa kwa kila upande iliishia kugonga mwamba na kurudi ndani ya uwanja. hadi kipindi Cha kwanza kinaisha hakuna timu iliyoona lango la mwenzake.DSC07059

Kipindi Cha pili kilianza na Hali haikubadilika sana hadi dakika ya 70 ambapo Timu ya Kariakoo iliweza kupata Goli la Kwanza baada ya Beki kucheza fyongo na kupeleka kilio langoni Mwao. Baada ya Goli hilo Timu ya Kariakoo Ilizinduka na kuweza kupata magoli mengine 2 ya haraka haraka na kufanya mchezo huo Kuisha kwa 3 – 0.

DSC07068Kabla ya mpira haujaanza wachezaji waliweza kukaa kimya kwa dakika mbili ilikuweza kutoa heshima kwa aliyekuwa mchezaji wa Kariakoo Fc ambaye amefariki dunia Alva Mmuni “mungu amuweke mahala pema”

Ligi hiyo Itaendelea Tena hapo Alhamisi kwa kuzikutanisha Timu za Kariakoo Fc na Captown Fc

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top