Unknown Unknown Author
Title: SIMULIZI:: NITAKUPENDA USIKU TU…!! SEHEMU YA NNE
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Chombezo: NITAKUPENDA USIKU TU Sehemu: 04 Mtunzi: Andrew Carlos Whatsap na Sms tu: 0713 133 633 Ilipoishia.. Likavua viatu vyake vya kuchom...

chombezo cover 1Chombezo: NITAKUPENDA USIKU TU
Sehemu: 04
Mtunzi: Andrew Carlos
Whatsap na Sms tu: 0713 133 633

Ilipoishia..
Likavua viatu vyake vya kuchomeka kisha likavisogelea vile vitoto. Havikuwa vikiogopa kwani ndio kwanza vilikuwa katika kunogewa katika kupuliza moshi wa sigara sambamba na kulitukana lile jimama langu.

Songa nayo sasa…
Niliendelea kukodoa mimacho utadhani naangalia picha bandani. Siyo picha ya kupigwa la hasha! ni picha za video tena zile za kuingia kwa kiingilio cha shilingi mia moja mpaka shilingi mia mbili na zile za kikubwa ambazo zilikuwa zikijulikana kwa jina la picha za ‘pilau’ au X zenyewe zilikuwa kati ya mia tau hadi mia tano. Uhondo ulioje kushuhudia mipaja hadharani nje nje tena ikijifunua pasipo kulazimisha wee acha tu.

Mawazo yaliniteka, yakaniteka, yakaniteka tena haswa kisha yakanirudisha mpaka mbele ya macho yangu nakuangalia kinachoendelea. Kumwangalia jimama aliyekuwa ameniachia vito vyake vya thamani nakuvifuata visichana vidogo vilivyokuwa vikijiuza miili yao. Vilivyokuwa vimeshamchambua jimama langu matusi ya nguoni. Havikujali. Vingejali nini wakati vilishakula kiapo cha kutokumuogopa mwanamke mwenzao yoyote pindi wawapo mawindoni?

“ Haya nyie vinyago mlikuwa mkiongea nini?” Aliongea yule jimama.
“Kinyago wewe na yule mpumbavu mwenzako!”
Kwani anataka nini huyu tumzime kwa sigara sisi” Kalidakia kasichana kadogo kakiizima sigara kwa kutumia skuna yake iliokuwa imechongoka kwa maeneo ya mbele. Hakakuwa na nguvu kwa muonekano wake. Kilivalia kisketi kifupi kilichokuwa kimezibwa na mtandio kiunoni. Lakini hata sikuelewa ni kitu gani kilichokuwa kikimfanya kujiamini kiasi kile, nilifikiri sana huenda hata kuwepo kwa wenzake wengi ndio kitu kilichokuwa kikimpa kiburi. Kikavua mtandio wake nakuutupa pembeni yake.

Alichokifanya yule jimama alikishika vilivyo kile kisichana. Vile vingine vyote vikaanza kutoa makelele ya mbwembwe pasipo kuweza kumsogelea tena yule jimama. Nikajisogeza kwa karibu japo kwenda kumchukua yule jimama aachane navyo tu lakini kitendo cha kusogelea kwa kwaribu vile visichana woga ukawajaa. Vikadhani sasa na mimi nitakuwa nimeudhika.

Mwili wangu uliokuwa umekomaa kwa kuwa na misuli kuanzia mikononi mpaka miguuni kwa kulima vitunguu na nyanya nyumbani kwetu Iringa ndio uliwaogopesha sana. Vikaanza kutawanyika kila mmoja kutafuta njia yake nakujiondokea. Nikamsogelea yule jimama.

“Achana navyo havina inshu hivyo!! chukuwa vitu vyako twende”
“Unasemaje na wewe?”
“Chukuwa vitu vyako twende tu achana nao hao”

Mwanzoni jimama lilionesha kama kutokunielewa lakini likakaa sawa. Likakiachia kile kisichana nguo ambayo ilikuwa imeng’ang’ana haswa na mikono yake.
Likachukuwa vitu vyake kwangu nakuvivaa.

“Umesema ni mtaa gani kwako”
“Tumeshakaribia kwani kwa hapa napafahamnu kabisa nilishawahi kupita sana, tukikunja kile kichochoro cha upande wa kule tutakunja tena ndio mtaa huo huo.”
“Twende”

Tulitoka pale uku lile jimama likinishika mkono na sikujua kwanini lilinishika mkono kwa nguvu zile sijui ndio lilijua huenda nikalikimbia. Kiakili hakuna. Kama ningelitaka kulikimbia ningeweza kufanya toka mwanzo aliponiachia tu vitu vyake. Tukaanza kukatiza kichochoro kimoja baada ya kingine. Hapakuwa na umbali sana kufikia getto niliokuwa nikiishi. Sikuwa muoga kutokana na chumba changu na hata wapangaji kutokuwa na mazoea na mimi. Na hii ni kutokana na kazi yangu. Kazi ya kushinda ndani siku nzima nikijifungia ndani nakutengeneza kahawa yangu na ikifika jioni kuchochea moto nakuosha vijikombe vya kahawa nakuingia mtaani. Hata mwenye nyumba mwenyewe sikuweza kumfahamu zaidi ya pesa yangu ya kodi kuwa nikimpatia mtoto wake tu.

“Mhh kumbe unakaa mbali hivi,”
“Ndio lakini tushafika!”
“Vigodoro hivyo!! sherehe haziwahusu mmevamia tu lakini kwa leo unabahati kukutana na tinginya kama mimi na umeona raha zake”
Likakenua meno uku likinitingishia makalio yake kiuchokozi. Tukatimba kwangu!!
“Ndio hapa, karibu najisikie uko nyumbani”
“Ndio kwako hapa?”
“Ndio”
“Kwako au kwenu”
“Kwangu nimepanga ingia wala usivue viatu”

Likazama kama msemo wa vijana wa siku hizi wasemavyo. Udogo wa chumba changu ulimfanya kupata tabu mule ndani. Kakitanda kadogo kakuunga na madumu ya maji kwa chini chaga zisiweze kupasuka ndicho alichokalia. Mwanzoni niliogopa sana. Nilijua tu naelekea kuumbuka. Kuumbulka kwa kulemewa kwa kitanda changu nakujikuta akizama mpaka chini lakini haikuwa hivyo.

“Sasa hapa, mhhh kweli ndio maana huna hata mke, unaishije chumba kidogo joto kali hewa nzito”
“Ndio maisha hayo nilioanza usijali mambo yanabadilika”
“haya nishapajua naenda”
“Sawa unaenda lakini ujue mpaka sasa sijakujua jina lako”
“Naitwa Mash, ni jina niliokulia nalo mtaani kwetu kote kule kutokana na mtoto nilivyojaaliwa. ndio wakanitungia jina la ‘Mashallah’ kifupi Mash.”
“Kweli umejaliwa Mash”
“Haya naaga tena nataka kwenda mwenzako”

Aliongea huku akiniangalia mara mbili mbili kana kwamba kunakitu amesahau. Alinyanyuka nakutaka kukaa tena. Akanyanyuka tena nakunisogelea mpaka karibu. Kisha akanong’ona kitu.

“Mashine yangu nitunzie kesho nitakuja kuitumia lakini nitakuja usiku tu”

Sikuwa na jinsi zaidi ya kumuitikia tena kwa kichwa kumuonesha kuwa nimekubaliana naye. Kimtazamo hakuonesha kabisa kuridhika na maneno yangu ya kumkubalia kirahisi hivyo.

“Nikwambie kitu Seif”
“Nambie”
“Nipe kwa mara ya mwisho basi mashine yako”

Kabla hajamalizia kusema lolote alinivagaa na limwili lake lote. Mdomo wake akanisogezea kwa karibu sana nakutaka ndimi ziweze kugusana. Mikono yake moja kwa moja akaisogeza mpaka chini kwa kasuku wangu ambaye ndio kwanza alikuwa akihesabu moja na moja kupata mbili anashindwa kusimama. Akihesabu mbili na mbili kupata nne bado alishindwa kabisa. Kifupi hali ilikuwa ile ile kwake. Aliweka kamgomo kwa muda. Mgomo wa kutokubali kusimama kabisaa.

“Usinifanyie hivyo Seif ujue hujanimalizia kabisa”
“Hata mie nashangaa ni yenyewe tu ndio inaleta magumashi”
Likanuna!!. Domo likapindua kuonesha kama limesusa kwa muda. Likaachana na kasuku wangu nakuniangalia mwa mara nyingine.
“Haya nisindikize”

Nilifungua mlango wangu nakutoka kwa utaratibu kama nyumba ya gesti kumbe ni kwangu. Sikutaka kwa muda kama huu kuwe na kelele kutokana na usiku kuingia na wote wapangaji walionesha kuwa kimya vyumbani mwao.

“Wewe ishia hapo hapo mie nshafika. Tutaonana kesho narudi kazini mimi”
“Haya poa kesho!”

Sikutaka hata kuuliza ni kazi gani anafanya japo nilihisi tu atakuwa akijiuza kutokana na mazingira aliyokuwa akiishi. Pili maneno yake aliokuwa akiyaongea kwa Jof pindi alipobisha hodi kwake yalinitia wasiwasi sana. Nilibaki nikimkodolea macho kumuangalia kwa upande wa nyuma kwa jinsi alivyokuwa kweli ameumbika uku kichwa changu akikiacha katika changamoto kubwa sana.

Sikutaka kabisa kuamini kama kweli jimama kama lile leo hii limeingia kwangu kiulaini kivile. Nilihisi huenda basi itakuwa ni ndoto lakini kila nikiyapikicha macho yangu nakuyafungua jibu lilliendelea kubaki pale pale kuwa ni ukweli kabisa nimetoka kuwepo na jimama.
***********

:: Sasa picha kamili ndio kwanza linaanzia hapa ule wote ulikuwa ni kama utangulizi tu!
Unavyodhani ni nini kitaendelea hapo kati ya Seif na Jimama ‘Mash’?
:: LIKE nyingi na COMMENT bila kusahau SHARE ndizo zinafanya Chombezo hili kuwa likitoka kila siku na kwa muda muafaka hapa. Hakika si ya kukosa hii.
::: ANGALIZO :::
Chombezo hili litakuwa likitoka kila siku kuanzia saa MOJA KAMILI ASUBUHI hapa hapa.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top