Lile penzi la mastaa wawili ambalo lilikuwa gumzo hapa mjini(Dar) na Tanzania mzima la wasanii wetu wawili ikiwemo yule wa muziki wa Bongoflava Naseeb Abdul_Diamond na Wema Abraham Sepetu limeonekana kupata doa baada ya anayeitwa kidudu mtu na Wema kuliingilia penzi la wawili hao.Diamond alikuwa akishoot video ya
wimbo wake mpya unaojulikana kama Mawazo ambamo kwenye video hiyo ataonekana mwanadada anayefahamika kama Jokate Mwegelo ambaye alikuwa miss Tanzania namba 2 mwaka 2006,mwanadada huyo inasemekana baada ya kumalizika kwa kazi ya kushoot video hiyo alizama penzini kwa Diamond hivyo kumfanya wema akose haki yake ya msingi kutoka kwa Diamond.Nanukuu kutoka kwa Wema "Baada ya kufanya shooting ya video walichukuana hadi hotelini ambako walikaa kwa siku nne hadi mimi nilipowafuma" alikuwa akilalamika Wema alipokuwa akihojiwa na Zamaradi wa Clouds TV.
Dah hyo tit for tati. Kumbe yauma eeeh mwache ale bhata nae kwan wewe umekula sana.
ReplyDelete