WANANCHI WATAKIWA KUTOA MAWAZO YAO KATIKA MCHAKATO WA KATIBA

WANANCHI mkoani Lindi wametakiwa kupuuza kauli za baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa wanao washawishi kutoshiriki kwenye mchakato wa kuchangia maoni yao juu ya uundaji wa katiba mpya unaotarajiwa kufanyika nchini kote hivi karibuni .
 image Ushauri huyo umetolewa na makamu wa kwanza wa rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Maalima Selfu Sharifu Hamadi wakati akizungumza kwa nyakati tofauti kwenye mikutano ya hadhara wilaya Lindi, na Kilwa katika vijiji vya Njinjo, Chumo.
Selfu alisema nchi yetu inaingia kwenye zoezi zito la mchakato wa uundaji wa katiba, ambayo inatarajia kufanikiwa baada ya wananchi kuchangia mawazo yao juu ya mambo gani wanataka yawepo katika katiba hiyo kwa ajili ya maedeleo yao ya miaka ijayo.
Alisema kuwa kuna baadhi ya viongozi ambao hawaitakii mema nchi yetu wanapita kila kona kwenye misikiti na makanisa kuendesha kampeni zisizo halali za kuwashawishi wananchi wasijitokeze kwenye mchakato wa kuchangia mawazo katika uundaji wa katiba hiyo mpya kwa lengo la kudhofisha zoezi hilo kwa maslahi yao binafsi.
Self alisema ni vyema wananchi wakatumia nafasi hiyo adimu kwao ambayo ikishapita haiwezi kupatikana tena, na hivyo watakuwa wamepoteza haki yao ya kikatiba ya kutoa mawazo yao ambayo yangewezakuboresha uundaji wa katiba hiyo mpya.
Ameonya kamwe wasikubali kurubuniwa na baadhi ya viongozi wenye uroho wa madaraka ambao wanataka kuingia ikulu kwa kumwaga damu za wananchi wasio na hatia kwa wanawashawishi kuandamana kupinga mchakato huo usiweze kufanikiwa.
Self pia amevitaka vyama vya siasa nchini kuondoa tofauti zao za kisiasa ili waweze kuwahudumia wananchi katika mambo yao ya kuwaletea maendeleo, kwani ameeleza kuwa siasa sio ugovi , uhasana , au mfarakano baina ya vyama au ndugu kwa ndugu.
Alisema mafanikio yaliyopatikana Zanzibar ya uundaji wa serikali ya kitaifa ni juhudi za pamoja kati ya chama cha wananchi (Cuf ) na chama cha mapinduzi (CCM)kwa kuwa na umoja shikamano ndani ya vyama hivyo kwa maslai ya wananchi.
Aidha alieleza kuwa kwa kipindi kifundi cha serikali ya kitaifa tayari wananchi wa visiwa hivyo wameanza kufaidika kwa kupata soko la uhakika na bei nzuri ya zao la karafuu kutoka shs 3000 kwa kilo hadi 15,000 , huku watumishi wa idara za serikali wakishuhudia kupata ongezeko la mishahara ya kwa asilimia 25.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post