Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameapishwa rasmi kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika sherehe zilizofanyika leo, Novemba 3, 2025, katika Uwanja wa Gwaride, Ikulu Chamwino mkoani Dodoma.
Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi wa kitaifa, viongozi wa dini, wanadiplomasia, pamoja na wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya nchi waliokusanyika kushuhudia tukio hilo la kihistoria.
Baada ya kula kiapo, Dkt. Samia ameahidi kuendeleza dira ya maendeleo, kudumisha amani, umoja na mshikamano wa kitaifa, huku akiwasisitizia Watanzania kuendelea kushirikiana katika kujenga Taifa lenye ustawi na haki kwa wote.
Tags
HABARI ZA KITAIFA


