Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ashiriki kwenye hafla ya utoaji tuzo za Wasanii wa Komedi Tanzania (Tanzania Comedy Awards) katika ukumbi wa The Super Dome, Masaki Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 22 Februari, 2025
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akifurahia jambo pamoja wa wageni mbalimbali wakati wa hafla ya utoaji wa Tuzo za Wasanii wa Komedi Tanzania (TCA) katika ukumbi wa The Super Dome, Masaki Jijini Dar es Salaam tarehe 22 Februari, 2025.
Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam.
February 22, 2025 ulikuwa ni Usiku wa Tuzo za Ucheshi (Tanzania Comedy Awards - TCA) na mgeni rasmi wa tuzo hizo alikuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika ukumbi wa Super Dome Masaki jijini
Dar es Salaam
Rais Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Serikali itaendelea kuwashika mikono wachekeshaji ili waweze kufika Kimataifa. ameongeza dhamira yake ni kuona vipaji vinaendelezwa.
Pia Rais Samia amesema binadamu kutofautiana kupo kwa sababu ya makabila mbalimbali ila ametaka watu wasitofautiane kama Watanzania, viuogomvi ugomvi haviwapi tija.
Katika tuzo hizo washindi waliopatikana ni kama ifuatavyo
- Best Funny Kid of the Year – Dogo Sele
- Best Breakthrough Comedian of The Year - Mzee wa Mpimbwe (Azaboi)
- Best Comedian Actor of The Year – Joti (+ Milioni 5)
- Best Upcoming standup Comedian – Mambise
- Best Comedian Duo Of the Year – Steve Mweusi na Ndaro
- Best Male Digital comedian of the Year – TX Dullah
- Best Female Digital Comedian of th Year – Mama Mawigi
- Best Male Stand Up Comedian of the Year – Eliud Swamwel
- Best Female standup Comedian Of the Year – Neila
- Best TV Comedy Show of the year – KITIMTIM
- Best Comedy special of the Year – Jol Master (The Guy)
- Tuzo Maalumu “Game Changer” - Coy Mzungu
- Best Male Comedian Of the Year – Nanga (Babu Kaju)
- Best Female Comedian of the Year – Asmah Majed
- Best Funny Leaders of the Year – Makongoro Nyerere
- Best Comedian of the Year Peoples Choice – Leornardo
- Best Legend Choice of the year – Joti
- Tuzo ya Heshima “Hall of Fame” - King Majuto
Tags
HABARI ZA KITAIFA