NIJUZE NIJUZE Author
Title: KOCHA WA YANGA ATOLEA UFAFANUZI KIPIGO DHIDI YA IHEFU FC
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema leo wamepoteza mchezo dhidi ya Ihefu Fc kwa kuwa walifanya makosa ndani ya uwanja na sio kwa saba...

Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema leo wamepoteza mchezo dhidi ya Ihefu Fc kwa kuwa walifanya makosa ndani ya uwanja na sio kwa sababu alifanya 'rotation' ya kikosi chake

Katika mchezo huo uliopigwa uwanja wa Highland Estates, Mbarali Mbeya, Gamondi alibadili takribani wachezaji saba walioanza katika mchezo uliopita kwenye ligi ya mabingwa dhidi ya Al Merrikh

"Tumepoteza mchezo sio kwa sababu nimefanya mabadiliko ya kikosi, tumefungwa kwa sababu tulifanya makosa. Nafikiri bao la kwanza tuliwapa zawadi, tulizungumza mapema kuwa uwanja haukuwa rafiki kwetu hivyo tuepuke kucheza kwenye eneo letu lakini yakafanyika makosa ambayo yalipelekea tukafungwa"

"Bao la pili lilikuwa shambulizi la kushitukiza, hatukufanya vile ambavyo tulipaswa kufanya na kupelekea tukaadhibiwa. Kama tungepata ushindi leo hakuna mtu angezungumzia mabadiliko. Wakati mwingine ni muhimu kufanya mabadiliko haya kwa kuzingatia ratiba inayotukabili," alisema Gamondi

Yanga imepoteza mchezo wake wa kwanza wa ugenini dhidi ya Ihefu fc kwa bao 2-1 hii ikiwa ni mara ya pili katika historia ya vilabu hivyo kukutana kwenye ligi kuu ya NBC. Msimu wa 2022/23 Yanga ilifungwa kwa idadi sawa ya mabao na kupoteza UNBEATEN ya 49.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top