NIJUZE NIJUZE Author
Title: CHAMA KIKUU CHA LINDI MWAMBAO CHAUZA TANI 2500 KOROSHO GHAFI
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
Na Ahmad Mmow, Lindi. Chama kikuu cha ushirika cha Lindi Mwambao kilichopo mkoani Lindi, leo kimeuza tani 2,556 na kilo 151 za korosho ghafi...

Na Ahmad Mmow, Lindi.

Chama kikuu cha ushirika cha Lindi Mwambao kilichopo mkoani Lindi, leo kimeuza tani 2,556 na kilo 151 za korosho ghafi.

Akizungumza katika mnada huo uliofanyika leo katika kijiji cha Namupa, kata ya Namupa halmashauri ya Mtama, meneja mkuu wa chama hicho, Nurdin Swallah alisema kwenye mnada huo wa tano kwa msimu wa 2023/2024 tani 2,556 na Kilo 151 zimeuzwa.

Swallah alisema bei ya juu ilikuwa shilingi 1,701. Ambapo bei ya chini ni shilingi 1,500 kwa kila kilo moja. Huku akiweka wazi kwamba katika tani hizo 2,556 na  kilo 151, kilo  2,433 na kilo 58 niza daraja la kwanza na tani 123 na kilo 93 niza daraja la pili.

Alisema kwenye mnada huo jumla ya barua tisa za kampuni mbali mbali ziliomba kununua korosho hizo zilizopo katika maghala ya Nangurukuru, Bucco, Ilulu na Hazina.

Meneja mkuu huyo wa Lindi Mwambao alisema katika mnada wa nne uliofanyika katika kijiji cha Naukauka, AMCOS ya NANYUMU ziliuzwa tani 1,926 za daraja la kwanza, na tani  52 na kilo 481. Ingawa tani zilizonadishwa zilikuwa tani 2,414 na kilo 26. Ambapo bei ya juu ilikuwa shilingi 1,800 na bei ya chini ni shilingi 1,700 .

Katika hatua nyingine Swallah alisema fedha za malipo ya wakulima walizouza korosho katika mnada wa nne zimelipwa na wanunuzi. Huku akibainisha kwamba jumla ya fedha hizo ni shilingi 3,343,956,964 (3.34 bilioni).

Kwenye mnada wa leo korosho za daraja la pili zimenunuliwa kwa shilingi 1,210 kila kilo moja.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top