Jeshi la Polisi Mkoani Lindi limewatoa hofu wananchi Mkoani humu baada ya doria zao kuzua sitofahamu na mijadala mbalimbali kwa wananchi wakihoji ni kwanini Polisi wamekuwa wakionekana mitaani na Barabarani wakiwa na silaha.
LINDIYETU BLOG imezungumza na kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Lindi Pili Mande amesema, mwonekano wao mitaani pamoja na doria ni sehemu tu ya kuonyesha uwepo wao na utayari kwaajili ya kukabiliana na matukio yote ya uhalifu.
Pili Mande amewataka wananchi kuendelea na shughuli zao kama kawaida pasi kuwa na hofu huku akieleza ya kwamba doria hizo zimefanywa na zinaendelea kufanyika Mkoani kote.
"Wananchi wasiwe na wasiwasi kwanini jeshi la Polisi linafanya doria kwa ukubwa huu hii yote ni kuonyesha kuwa jeshi la Polisi Lipo na wananchi musiwe na taharuki yoyote" alisema Pili Mande
Doria hiyo iliyozua taharuki imewafanya wananchi kuwa na wasiwasi Mkubwa, Shabani Kikotokeki ambaye ni mfanyabiashara mkoani hapa ameomba ili kuondoa taharuki kwa wananchi na kuwafanya wasizungumze nadharia tofauti tofauti zenye kuwatisha watu zaidi, basi taarifa zitolewe kabla ya doria ili watu wafahamu ni jambo gani linaendelea.
"Hizi siku mbili tatu wananchi tulikuwa na taharuki kuona jeshi la Polisi likiwa na vifaa, magari wapo kwenye Oparesheni hivi ambayo ilitutia hofu kidogo kwasababu hatujazoea jeshi la Polisi kuwa katika hali kama hii..... Nafikiri si jambo baya endapo tutapewa taarifa kabla ya zoezi kutokea kwasababu wengi wetu hatuna elimu ya kujua kuhusu oparesheni kama zile" alisema Shabani Kikotokeki
Jeshi la Polisi limewataka wananchi wasiwe na taharuki yoyote na waendelee kufanya shughuli zao kwa amani. Tukio na hali ya doria wanayoitekeleza ni kuonyesha kuwa wakati wote wapo TIMAMU
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.