Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Afrika (CAF) limetangaza rasmi nchi za Tanzania, Kenya na Uganda kuwa muandaaji wa michuano ya AFCON 2027.
Kamati hiyo Tendaji ya CAF imetangaza uoamuzi huo leo Cairo,
Misri nah ii ni mara ya kwanza kwa nchi za ukanda wa Afrika Mashariki kuandaa
michuano hii toka ianze.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Samia Suluhu Hassan
ameagiza Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kuhakikisha inafanya maandalizi
mazuri ya AFCON 2027 ikiwemo kukamilisha kwa wakati na kwa ubora, viwanja
viwili vipya vya kisasa vya michezo Arusha na Dodoma
Kupitia Ukurasa wake rasmi wa Mtandao wa X, Rais ameandika:
"Tunamshukuru Mwenyezi Mungu tumefanikiwa kuwa wenyeji
wa michuano mikubwa ya soka Afrika (AFCON2027), tukishirikiana na Kenya na
Uganda. Nawapongeza nyote mlioshiriki kuhakikisha nchi yetu inapata fursa hii
adhimu. Nawaagiza Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kuhakikisha tunafanya
maandalizi mazuri, ikiwemo kukamilika kwa wakati na kwa ubora wa hali ya juu,
viwanja viwili vipya vya kisasa vya michezo Arusha na Dodoma".
Tunamshukuru Mwenyezi Mungu tumefanikiwa kuwa wenyeji wa michuano mikubwa ya soka Afrika (AFCON2027), tukishirikiana na Kenya na Uganda. Nawapongeza nyote mlioshiriki kuhakikisha nchi yetu inapata fursa hii adhimu. Nawaagiza Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kuhakikisha… pic.twitter.com/jhBQptTV5l— Samia Suluhu (@SuluhuSamia) September 27, 2023