AJIRA 550 KUTOLEWA KWA VIJANA MKOANI MTWARA

Takribani ajira 550 zinatarajiwa kutolewa kwa vijana wa Mkoa wa Mtwara kupitia kampuni ya ulinzi ya Asgard Security, katika kada mbalimbali. Vijana wametakiwa kuchangamkia fursa hizo ili kujikwamua kiuchumi.

Akizungumza, Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Bw. Samweli Magita, alisema nafasi hizo zinajumuisha walinzi wa kawaida, walinzi wa kutumia silaha, wasimamizi wa ofisi, wauguzi, madereva, watunza taarifa, wataalamu wa kuzima moto pamoja na watembea na mbwa (Dog Handlers).

“Tunahitaji vijana 550 kutoka kada tofauti. Watakaopatikana watapewa mafunzo kabla ya kuanza kazi. Kwa wanaotoka nje ya Mtwara, tumetenga makazi na tutagharamia usafiri pamoja na chakula hadi mishahara itakapoanza kulipwa,” alisema Bw. Magita.

Alifafanua kuwa nafasi hizo zinagawanyika kama ifuatavyo:

  • Walinzi wa kawaida: 300
  • Walinzi wa kutumia silaha: 50
  • Watunza taarifa: 10
  • Madereva: 20
  • Wauguzi: 5
  • Wasimamizi wa ofisi: 5
  • Wataalamu wa uzimaji moto: 20
  • Watembea na mbwa: Nafasi maalum

Mwombaji anatakiwa kuwasilisha:

  • Barua ya maombi
  • Barua kutoka serikali ya mtaa
  • Nakala ya kitambulisho cha NIDA
  • Picha mbili za pasipoti
  • Barua mbili za wadhamini waliothibitishwa na mwenyekiti wa mtaa

Kwa wanaopenda kuwasilisha maombi kwa njia ya mtandaoni, wanaweza kutumia barua pepe info@asgardsecurity.co.tz au kupiga simu kupitia namba zifuatazo:
0742373932, 0745146249, 0713482318, 0658385515, 0655957525, 0715397813.

Kwa walio Mtwara mjini, wanaweza kufika ofisi za kampuni zilizopo Rahaleo karibu na benki ya DTB. Maombi yanapokelewa kuanzia Aprili 17 hadi Mei 17, 2025.

Kwa walioko nje ya Mtwara:

  • Dar es Salaam: Ofisi kuu zipo Mwembeni, Kinyerezi – kituo cha Mwembeni
  • Mwanza: Ofisi ipo kwenye jengo la zamani la Idara ya Madini, Nyumba Namba 3

Kwa upande wake, Afisa Rasilimali Watu wa kampuni hiyo, Bw. Mfumbwa Mzige, aliwahimiza vijana kutokata tamaa katika kuomba kazi hizo.

“Hata kama huna kiwango cha juu cha elimu, muonekano wako unaweza kukupa nafasi. Jambo muhimu ni kufuata masharti yaliyowekwa na kuhakikisha barua yako ya maombi inaeleza aina ya kazi unayoomba. Pia hakikisha una barua mbili za wadhamini kutoka kwa watu waliothibitishwa na serikali ya mtaa,” alisema Mzige.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post