Jeshi la Polisi Tanzania limetangaza nafasi za ajira kwa vijana wa Kitanzania wenye sifa zinazohitajika, ili kujiunga na jeshi hilo kwa mwaka 2025.
Kwa mujibu wa tangazo rasmi lililotolewa na Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, waombaji wanapaswa kuwa raia wa Tanzania kwa kuzaliwa, wenye umri wa kati ya miaka 18 hadi 25 kwa wenye elimu ya kidato cha nne hadi sita na Astashahada.
Waombaji wenye elimu ya Stashahada na Shahada wanatakiwa kuwa na umri wa hadi miaka 30.
Sifa za Muombaji:
- Awe raia wa Tanzania kwa kuzaliwa na wazazi wake wawe raia wa Tanzania kwa kuzaliwa.
- Awe amehitimu kidato cha nne au sita kati ya mwaka 2019 hadi 2024
- Kwa wenye kidato cha nne, wawe na ufaulu wa daraja la kwanza hadi la nne.
- Kwa wenye kidato cha sita, wawe na ufaulu wa daraja la kwanza hadi la tatu.
- Awe na kimo kisichopungua futi tano na inchi nane (5’8”) kwa wanaume, na futi tano na inchi nne (5’4”) kwa wanawake.
- Awe na nidhamu, afya njema, na asiwe na rekodi ya uhalifu.
- Awe tayari kufuata maadili na kanuni za Jeshi la Polisi.
- Awe na cheti halali cha kuzaliwa na kitambulisho cha taifa au namba ya NIDA.
- Asiwe na michoro ya kudumu mwilini (tattoo).
Utaratibu wa Kutuma Maombi:
Waombaji wote wanatakiwa kuandika barua ya maombi kwa mkono na kuiwasilisha kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi, S.L.P 961, Dodoma. Barua hiyo iambatane na nakala ya vyeti vya elimu, cheti cha kuzaliwa, na kitambulisho cha taifa au namba ya NIDA.
Pia, maombi yanaweza kufanyika kwa njia ya mtandao kupitia mfumo wa Tanzania Police Force – Recruitment Portal unaopatikana kupitia tovuti ya Jeshi la Polisi: https://ajira.tpf.go.tz.
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 04 Aprili 2025.
Kwa maelezo zaidi, waombaji wanashauriwa kufuatilia tangazo rasmi kupitia vyanzo vya Jeshi la Polisi Tanzania.