Na. Farhan Kihamu Jr.
RAIS PEREZ wa Real Madrid aliwahi kuulizwa swali kwanini anajaza watoto wengi wadogo Real Madrid ambao uhakika wa namba ni mdogo, akawaambia Waandishi ukishaitaja Madrid maana yake ni timu kubwa yenye wachezaji wakubwa.
Rais akawauliza wachezaji wadogo wanatrain na wachezaji
gani? Majibu yakawa wachezaji wakubwa, akauliza tena maisha ya Mchezaji
anatumia muda mwingi mazoezini ama mechi? Majibu yakawa mazoezi ya mpira wa
miguu, maana yake anafaidi vingi zaidi mazoezini.
Nikamkumbuka Brahim Diaz alivyotoka Real Madrid na kwenda
Milan alikuwa hatari lakini alikuwa bench Madrid, nikamkumbuka Casemiro kutoka
Real Madrid akaenda Porto, Alvaro Moratta na Marco Asensio, yes nikaelewa point
ya Perez.
Nawatazama Vijana wadogo kama Denis Nkane, Abou Mshery,
Nickson Kibabage, Crispin Ngushi, Kibwana na Clement Mzize ndani ya Yanga
Afrika! To me hawapaswi kuwa na presha na Yanga hawapaswi kuacha kusign young
talents, ni faida kubwa sana kwa Taifa! Kupitia timu kubwa Mchezaji anaandaliwa
kuwa mkubwa.
Unamkumbuka Eric Johora the Keeper? Alikuwa anaozea bench tu
Yanga lakini anatrain na Djigui Diarra! Ameondoka kwenda Geita baada ya misimu
miwili, ameonesha kiwango bora na ameitwa National Team, Abou anakaa bench
Yanga ila akiwa fit huwa anaitwa National team! Nickson sio regular lakini
anaitwa National Team!
Hii sio kuuwa vipaji vya Wachezaji vijana bali kuwakuza
kiakili na kimchezo, ni kuliponya taifa! Mchezaji anapotakiwa na timu kubwa
acha aende, stori za kukaa bench hazimake sense.