Na.Elimu ya Afya kwa Umma.
Mganga Mkuu Mkoa wa Rukwa Dkt. Ibrahim Isack ameipongeza Wizara ya Afya pamoja na wadau mbalimbali ikiwemo Shirika la Afya Duniani( WHO), Shirika la Kuhudumia Watoto Duniani( UNICEF) pamoja na Save the Children kwa kuweka nguvu za pamoja kufanikisha Kampeni ya Chanjo ya Matone dhidi ya Polio.
Dkt.
Isack ametoa pongezi hizo Mkoani Rukwa ikiwa Uzinduzi wa Kampeni ya
Chanjo ya Matone dhidi ya Polio kitaifa ulifanyika Mkoani humo huku
walengwa ilikuwa ni watoto walio na umri chini ya miaka 8 katika mikoa 6
ya Rukwa, Katavi, Kagera, Kigoma, Mbeya na Songwe.
"Kwa
kweli Wizara ya Afya pamoja na wadau ikiwemo WHO, UNICEF na Save the
Children wamekuwa na mchango mkubwa hususan suala uwezeshaji na
uelimishaji kwa jamii"
Naye
Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Sumbawanga Mkoani Rukwa Catherine
Mashalla amesema hamasa ya Elimu ya Afya kwa Umma imekuwa na mchango
mkubwa kufikia jamii kupata chanjo ya Polio kwa watoto.
"Tunashukuru
tumekuwa tukihamasisha jamii na Elimu ya Afya kwa Umma pamoja na Mpango
wa Taifa wa Chanjo wametusaidia sana kupita sehemu mbalimbali na
kutumia wimbo wa hamasa"amesema Mashalla.
Mratibu
wa Chanjo Mkoa wa Rukwa Ndenisia Ulomi amesema wadau wamesaidia katika
ufuatiliaji wa magonjwa yanayozuilika kwa chanjo ambapo jumla ya watoto
546, 026 wamepatiwa chanjo Mkoani Rukwa.
"Tumeshirikiana
na Wizara ya Afya pamoja na Wadau ambapo katika halmashauri ya Wilaya
ya Kalambo lengo ilikuwa ni kuchanja watoto 80,486 waliofikiwa ni
watoto 111,524 sawa na asilimia (138.56%), Nkasi DC lengo ni kuchanja
watoto 109,514 na waliochanjwa ni watoto 145, 234 sawa na asilimia
132.62%, Sumbawanga DC lengo ni watoto 118,071 na waliochanjwa ni watoto
175,165 sawa na 148.36% na Sumbawanga MC lengo lilikuwa watoto 83,811
na waliochanjwa ni watoto 114,103 sawa na asilimia 136.14%"amesema.
Naye
mwakilishi wa Save the Children George Sungwa amesema Wizara ya Afya,
Ofisi ya Rais TAMISEMI ,Mkoa wa Rukwa pamoja na wadau wengine wamekuwa
na mchango mkubwa katika Kampeni ya Polio.
Alex
Mwembezi pamoja na Rusia Swaila ni miongoni mwa wakazi wa Mkoa wa Rukwa
ambapo wamesema kutokana na hamasa ya Elimu ya Afya kwa Umma wamekuwa
na uelewa juu ya chanjo ya matone dhidi ya ugonjwa wa Polio ikiwemo
kuzuia kupooza.
Ikumbukwe
kuwa Kampeni ya chanjo ya matone dhidi ya ugonjwa wa Polio ilianza
Septemba 21-24, 2023 katika mikoa 6 ya Rukwa, Kagera, Katavi, Kigoma,
Mbeya na Songwe na matarajio ya kuchanja ni zaidi ya watoto milioni
tatu.
Tags
HABARI ZA KITAIFA