YANGA YATUA MTWARA TAYARI KUWAKABILI NAMUNGO FC

MSAFARA wa wachezaji 21 wa Yanga umesafiri saa 11:00 alfajiri ya leo kuelekea mkoani Lindi, kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Namungo Kwa kutumia shirika la ndege la Precision.

Msafara huo umetua uwanja wa ndege wa Mtwara kisha watapumzika hotelini mkoani Mtwara na kufanya mazoezi jioni ya leo kabla ya kuanza safari ya basi kuelekea Ruangwa, Lindi hapo kesho.

yangasc-317991543-710996347059914-9097973598332889797-n

Wachezaji walio kwenye msafara huo ni:

Djigui Diarra, David Bryson, Erick Johola, Kibwana Shomary, Joyce Lomalisa, Djuma Shabani, Ibrahim Abdullah, Dickson Job, Yanick Bangala, Khalid Aucho, Gael Bigirimana, Zawadi Mauya, Jesus Moloko, Tuisila Kisinda, Denis Nkane, Clement Mzize, Aziz Ki, Bernard Morrison, Fiston Mayele, Dickson Ambundo na Feisal Salum.

Kiungo Salum Abubakari na winga Farid Mussa watakosekana kwenye mchezo huo kwa sababu ya majeraha.

yangasc-318012009-135493429305615-325565533735939901-n

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post