JOB ASAKA REKODI MAJALIWA STADIUM

BEKI Dickson Job amerudi kwenye kikosi cha Young Africans baada ya kumaliza adhabu yake ya kadi tatu za njano iliyompelekea kukosa mchezo dhidi ya Tanzania Prisons.

Kurejea kwa Job bila shaka kunamuweka kwenye nafasi nzuri ya kupata nafasi ya kucheza mechi ya Jumatano dhidi ya Namungo, mchezo utakaopigwa katika uwanja wa Majaliwa, Ruangwa.

Job-1320x1320

Mchezo huu Job anautamani kwa sababu tangu ajiunge na Wananchi, beki huyu kutoka Morogoro hajawahi kupoteza mchezo kwenye uwanja huo.

“Huu uwanja wa Majaliwa umekuwa na bahati na mimi, nimekuja hapa na Yanga mara mbili na zote sijapoteza. Ni furaha kwa mchezaji kucheza mechi kubwa ugenini na ukaondoka na ushindi.

“Niwaombe mashabiki wa Yanga kuja kwa wingi uwanjani kwa ajiili ya kutushangilia na kutupa hamasa ya kumaliza mzunguko wa kwanza tukiwa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu,” alisema Job

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post