YANGA YAMALIZA KIBABE MZUNGUKO WA KWANZA YAICHAPA NAMUNGO FC 2-0

Mpira umemalizika katika dimba la majaliwa na ni Yanga aliyeondoka na alama tatu dhidi ya wenyeji wauaji wa kusini Namungo Fc kwa jumla ya magoli 2-0.

yangasc-318519941-454528266859113-2079624386839848316-n

Yannick Bangala ndiye aliyeanza kuzifumania nyavu za Namungo dakika ya 40 akimalizia mpira uliomshinda mlinda lango wa Namungo baada ya mpira wa kutenga uliopigwa na Stephan Aziz Ki.

yangasc-318686448-710234614017381-7524363735722588866-n

TK Master akaona isiwe shida akaweka chuma cha pili kwa Yanga baada ya kumlaghai golkipa kwa kutishia kupiga krosi na badala yake akaukwamisha nyavuni mnamo dakika ya 83 ya mchezo huo

yangasc-318472013-1177904233155685-6147236097691778235-n

Kwa matokeo hayo Yanga inasalia kileleni mwa Msimamo wa Ligi Kuu ya NBC baada ya michezo 15 ikiwa na alama 38.

Ligi Kuu Tanzania Bara imemalizika mzunguko wa kwanza baada ya mechi mbili za leo na hii ndio Hali halisi ya Msimamo wa Ligi ulivyo:

Soccer-Table-Graphic

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post