YANGA YAISHUSHIA KIPIGO SINGIDA BIG STARS 4-1 | NBC PL

Yanga Sc wamerejea kileleni kwa kuiadhibu Singida Big Star kwa mabao 4-1 kwenye ligi kuu Tanzania Bara, mchezo ambao ulipigwa kwenye dimba la Benjamin Mkapa jijini dar es Salaam,

Stori kubwa kwenye mchezo huo ni Fiston Kalala Mayele ambaye amefunga mabao matatu, Hat trick baada ya kukaa muda mrefu bila kuzifumania nyavu kwenye ligi kuu inayoendelea huku goli lingine likifungwa na beki Kibwana Shomari.

Singida Big Star bao lao pekee lilifungwa na Meddie Kagere ambaye nae amekua hana muendelezo mzuri wa ufungaji huku kwenye ligi hii ya NBC amefunga mabao mawili tu hadi hivi sasa na kwa upande wa Fisto Mayele akifikisha mabao sita ndani ya ligi msimu huu.

Yanga sasa Itasafiri hado Makao makuu ya Nchi ya Tanzania Dodoma Kuikabili Dodoma Jiji katika muendelezo wa mechi za Ligi Kuu ya NBC ambayo itachezwa Novemba 22, 2022.

yangasc-315970263-8334702703269703-4267810221013838672-n yangasc-316004602-129038173289864-8406288761336459803-n yangasc-316054799-539397551532358-7992493182850922729-n yangasc-315779045-1071958146807324-8168481310572933541-n

Soccer-Table-Graphic

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post