MAKAMBO NJE WIKI SITA

MSHAMBULIAJI wa Young Africans Kipenzi cha mashabiki wa klabu hiyo Heritier Makambo atakua nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki sita baada ya kugundulika amevunjika mfupa mdogo wa kifundo cha mguu.

Akizungumzia kadhia hiyo Daktari wa Yanga, Moses Etutu alisema vipimo vimeonyesha Makambo amepata jeraha hilo na itamchukua wiki sita kuwa nje ya uwanja akijiuguza.

“Alikuwa akilalamika sana kuwa anasikia maumivu makali akicheza, ikatulazimu kumfanyia vipimo na ikagundulika kuwa amevunjika mfupa mdogo kwenye kifundo chake cha mguu.

“Baada ya kugundua hilo tumemuanzishia ratiba ya matibabu ambayo inaweza kumchukua hadi wiki sita kuwa nje ya uwanja akiuguza jeraha lake,” alisema Dokta Etutu.

A30-I0106-1-1024x975

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post