Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Imeiondolea Klabu ya Singida Big Stars (SBS) adhabu ya kufungiwa kusajili,
Kamati imesema badala ya adhabu hiyo, klabu imepigwa faini ya TZS milioni moja ambayo inatakiwa kulipwa kabla ya dirisha dogo la usajili kufunguliwa Disemba 15 mwaka huu
Uamuzi huo umefanywa leo Novemba 29, 2022 na kamati mara baada ya kupitia hoja za SBS katika mombi yao ya marejeo (review) kuhusu uamuzi wa awali wa kuifungia kusajili
Taarifa imeeleza kuwa iwapo SBS haitalipa faini hiyo ndani ya muda uliowekwa, adhabu ya kufungiwa kusajili itabaki palepale
Kamati ilitoa adhabu hiyo kwa Singida Big Stars baada ya kukiuka kanuni za usajili wa wachezaji kwa kusajili wachezaji wenye mikataba na klabu zingine Oktoba 7, mwaka huu.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.