Klabu ya Yanga imepoteza mchezo wake wa kwanza wa ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya IHEFU SC na kuzima ndoto ya kufikisha rekodi ya UNBEATEN ya 50 katika mchezo ulipigwa katika uwanja wa Highland Estastes Mbalari Jijini Mbeya.
Yanick Bangala Litombo alianza kuifungia Yanga Goli la kuongoza dakika ya tisa akifunga bao lake la kwanza msimu huu akiwa na Yanga, amefunga baada ya kucheza michezo minane pasipo kufunga, bao hilo limetengenezwa na mlinzi ghali wa kushoto Joyce Lomalisa ambaye hili ni bao la tatu anatengeneza.
Never Tegere alifunga goli la kusawazisha dakika ya 39 huku Lenny Kissu akitia kambani goli la pili na laushindi kwa IHEFU dakika ya 62 ya mchezo na kufanya matokeo kuwa 2-1 hadi kipyenga cha mwisho cha mwamuzi wa kati.
Kwa Matokeo haya IHEFU wanapanda kutoka nafasi ya 16 hadi nafasi ya 13 ikiwa na alama 11 ikiwa imecheza michezo 14 sawa na Ruvu Shooting wakiwa na tofauti ya magoli ya kufunga na Kufungwa.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.