FEISAL SALUM KUIKOSA MBEYA CITY LEO

Young Africans inaenda kucheza mchezo wa 12 Ligi Kuu msimu huu, wakicheza dhidi ya timu ngumu kutoka jiji la Mbeya, Mbeya City FC mchezo unaopigwa katika dimba la Benjamin Mkapa leo hii novemba 26 majira ya saa 12:15 jioini. 


Kocha msaidizi wa Young Africans ameweka wazi kuwa kiungo fundi Feisal Salum ‘feitoto’ atakosekana katika mchezo wa leo sababu ikiwa ni kuwa na Kadi tatu za njano.

“Tuna wachezaji walikosekana mchezo uliopita, hata kesho kuna wachezaji tutawakosa, hii inatokana na ratiba ngumu ambayo inatulazimu kufanya mabadiliko. Baadhi ya wachezaji wamerejea kama vile Aziz Ki, Djigui Diarra, kutoka kwenye majukumu ya timu za taifa. Yannick Bangala nae amerejea baada ya adhabu yake kuisha lakini tutamkosa Feisal Salum kutokana na kadi tatu za njano.” Cedric Kaze

Young Africans inaingia kwenye mchezo huo wakiwa na rekodi nzuri ya kutokufungwa kwa mechi 48. Je Mbeya City wataweza kuwazuia Yanga? Dakika tisini zitajibu kitendawili hiki pale LUPASO Leo.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post