Watoto wawili wamefariki dunia na wengine 15 wamenusurika kifo baada ya kula chakula ambacho kinadhaniwa kuwa na sumu.
Taarifa hiyo imetolewa jana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Henry
Mwaibambe, wakati akizungumza na waandishi wa habari, amewataja
waliofariki kuwa ni Manyirizu Joseph (6) na Bertha Mateso (5) ambao wote
ni wakazi wa Ikobe wilayani Mbogwe.
Kamanda Mwaibambe amesema watoto hao na wengine waliojeruhiwa walikula
mabaki ya chakula (kiporo) ambacho ni wali na nyama ya kondoo na kuanza
kutapika pamoja na kuharisha.
Aidha, Kamanda huyo amesema hali ya manusura wanaendelea na matibabu
katika kituo cha afya Iboya wilayani Mbogwe mkoani humo na hali zao
zinaendelea vizuri.