REKODI MPYA YA DIAMOND PLATNUMZ

STAA wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz amepiga hatua nyingine kubwa katika kazi yake ya muziki na kuwa mwanamuziki wa kwanza Kusini mwa Jangwa la Sahara kupata subscribers milioni tano katika mtandao wa YouTube, kupitia chaneli yake ya YouTube. 


Kwa karibu anafuatwa na Rayvanny Akiwa na subscribers milioni 2.63, Harmonize akiwa na milioni 2.4, Davido akiwa na milioni 2.38, Burna Boy milioni 1.82 na Wizkid milioni 1.68.

Mafanikio haya ya sasa ya Diamond yanakuja yakifuata rekodi aliyoiweka mwaka jana (2020) baada ya wimbo wake maarufu ‘Waah‘ aliomshirikisha mwanamuziki wa Koffi Olomide wa DRC kutazamwa na watu milioni 1 ndani ya saa 8 baada ya kibao hicho kutoka.

Mondi aliivunja rekodi iliyowekwa na mwanamuziki wa Nigeria Davido baada ya kibao chake ‘Fem‘ kuwavuta watazamaji milioni moja ndani ya saa 9 tangu kibao hicho kilipoachiwa.

Aidha, Rekodi nyingine iliyowekwa na mwimbaji huyo ni kuwa msanii wa kwanza Kusini mwa Jangwa la Sahara kuwa na Watazamaji bilioni moja kwenye mtandao wa YouTube pekee.


 

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post