Ikiwa sehemu ya maandalizi kuelekea mchezo wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya KMC ambao utapigwa Jumamosi, April 10, Yanga April 6 ilicheza mechi ya kirafiki dhidi ya African Lyon inayoshiriki ligi daraja la Kwanza.
Wananchi wameondoka na ushindi wa mabao 3-0 yakipachikwa kupitia Fiston Abdulrazak, Michael Sarpong na Paulo Godfrey 'Boxer'.Ilikuwa ni mechi ya kirafiki ya ndani maalum kwa ajili ya kuziandaa timu zote kuelekea mechi za ligi kuu na ligi daraja la kwanza zitakazoanza kupigwa mwishoni mwa wiki.
Tags
MICHEZO