ONYANGO ANYAKUA TUZO YA LUIS MIQUISSONE

BEKI kisiki wa Simba raia wa Kenya, Joash Onyango, amekabidhiwa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi Machi wa kikosi hicho baada ya kupigiwa kura nyingi na mashabiki.

Onyango amewashinda Aishi Manula na Luis Miquissone kwenye kinyang’anyiro hicho cha kuwania tuzo hiyo inayodhaminiwa na Kampuni ya Emirates Aluminium Profi le.

Beki huyo anakuwa mchezaji wa pili kutwaa tuzo hiyo iliyoanza kutolewa Februari, mwaka huu na kubebwa na Luis. Mbali na kupewa tuzo, Onyango amekabidhiwa kitita cha shilingi milioni moja.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo Onyango alisema “Tuzo hii itaongeza morali kwangu na kwa wenzangu katika hali ya kuendelea kupambana kwa ajili ya miezi mingine ijayo.

Kwa upande wa Ofisa Mahusiano wa Emirates, Issa Maeda, amesema "Tutaendelea kutoa tuzo hizi hadi mwisho wa msimu, mambo yakiendelea kuwa mazuri, msimu ujao tunaweza kuwepo tena na kuongeza dau kufikia shilingi milioni tano".


 

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post