NIJUZE NIJUZE Author
Title: SAIDO, YACOUBA, JOB NA SARPONG HALI TETE YANGA
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
HALI bado ni tete kwa nyota wanne wa kikosi cha klabu ya Yanga, Saidi Ntibazonkiza ‘Saido’, Yacouba Sogne, Dikson Job na Michael Sarpong amb...

HALI bado ni tete kwa nyota wanne wa kikosi cha klabu ya Yanga, Saidi Ntibazonkiza ‘Saido’, Yacouba Sogne, Dikson Job na Michael Sarpong ambao wameshindwa kufanya mazoezi ya pamoja na wenzao kutokana na kusumbuliwa na majeraha.

Nyota hao ambao kwa ujumla wameifungia Yanga mabao 11 msimu huu (Yacouba 4, Sarpong 4, na Saido 3) wanasumbuliwa na majeraha ya nyama za paja pamoja na goti.

Saido na Yacouba waliumia kwenye michezo ya ligi, Job aliumia kwenye kambi ya Taifa Stars, huku Sarpong yeye akipata majeraha hayo mazoezini.

Meneja wa kikosi cha Yanga, Hafidh Saleh alisema wachezaji wote wa kikosi hicho wanaendelea vizuri na programu za mwalimu, isipokuwa nyota hao wanne ambao wamepewa programu maalum za mazoezi tofauti na wenzao.

“Hali ya kikosi chetu kiujumla ni nzuri, wachezaji wote wanaendelea na mazoezi chini ya kocha Kaze, isipokuwa nyota wetu wanne ambao ni; Saido, Yacouba, Sarpong na Job ambao wao bado wanasumbuliwa na majeraha na wanaendelea na matibabu pamoja na progamu tofauti za mazoezi kulinganisha na zile wanazofanya wenzao.

“Saido, Yacouba na Job wote wana majeraha ya nyama za paja, huku Sarpong yeye akiwa na majeraha ya goti ambayo aliyapata mazoezini.

“Hivyo timu yetu ya madaktari inaendelea kushirikiana na kocha wetu wa viungo Edem Mortotsi, kwa ajili ya kuhakikisha wanarejea katika hali yao ya kawaida kabla ya ligi kurejea,” alisema Hafidh.

 

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top