NIJUZE NIJUZE Author
Title: TUTACHEZA KILA MECHI KAMA FAINALI - KAZE
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
Baada ya watani zao Simba kulazimishwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Azam Fc hapo juzi, vinara wa ligi kuu ya Vodacom Yanga wana nafasi ya kuen...

Baada ya watani zao Simba kulazimishwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Azam Fc hapo juzi, vinara wa ligi kuu ya Vodacom Yanga wana nafasi ya kuendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi siku ya Jumamosi kama watapata ushindi dhidi ya Mbeya City.Mabingwa hao wa kihistoria watakwenda Mbeya huku wakifahamu ushindi kwenye mchezo huo utawafanya waongeze tofauti ya alama dhidi ya Simba kutoka alama tano na kuwa nane.

Kocha Mkuu wa Yanga Cedric Kaze amesema wanazichukulia mechi zote zilizobaki sawa na mechi za fainali, wakianzia na mchezo dhidi ya Mbeya City.

"Tunafahamu mchezo dhidi ya Mbeya Ciy hautakuwa mwepesi nadhani hata mechi nyingine zote zilizobaki zitakuwa hivyo hivyo"

"Tunapaswa kupambana katika kila mchezo ili kuweza kushinda," alisema Kaze.

Kulingana na Ratiba iliyotolewa na Bodi ya Ligi, baada ya mchezo dhidi ya Mbeya City, Yanga itarejea jijini Dar es salaam ambako itacheza mechi mbili dhidi ya Kagera Sugar na Mtibwa Sugar.

 


About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top