
Akidhibitisha tukio hilo, Kamanda wa Polisi mkoani Tabora Kamishina Msaidizi Hamis Suleiman, amemtaja marehemu kwa jina la Akihila Takahashi(49), akidai kuwa tukio hilo ni la kushangaza, na ni la kwanza mkoani Tabora mtaalamu na Raia wa Kigeni kujinyonga, huku akisema kuwa uchunguzi wa kina unafanyika.

Wakiongea na Lindiyetu.com kwa masikitiko eneo la tukio ambapo Mjapan huyo alijinyonga kwa kutumia kamba, baadhi ya wafanyakazi wenzake walioshuhudia mwili wa marehemu ukiwa umening’inia wamesema kuwa, jana yake walikuwa naye kazini kama kawaida.
Tags
HABARI ZA KITAIFA