MEYA MANISPAA YA LINDI AONGELEA SINTOFAHAMU YA TASMINI YA MRADI WA GESI MBANJA

Likong’o
Wakazi wa kijiji cha Mto mkavu na Likong’o, kata ya Mbanja Manispaa ya Lindi walalamikia wakati mgumu wa shughuli za kimaendeleo baada ya sitofahamu ya muda mrefu kutokana na tasmini ya mradi wa ujenzi wa kinu cha gesi uliopiita katika makazi yao.

Akiaongea na Lindiyetu.com mkazi wa eneo hilo amesema kuwa wananchi hadi sasa hawajui mahali pa kwenda na hawajui lini watapatiwa stahiki zao kwani muda uliopangwa umeshapita na bado haijaeleweka lini watakamilishiwa malipo hayo.

Akiongelea suala hilo Meya wa Manispaa ya Lindi Ndg Mohamedi Lihumbo alisema kuwa hatma ya wananchi hao bado inafanyiwa kazi na wananchi wasiwe na wasiwasi kwani watapewa stahiki zao na kuoneshwa mahali pakwenda ambapo patakuwa pamepimwa.

UNAWEZA KUSIKILIZA SAUTI ZAO HAPA CHINI
Previous Post Next Post