MBUNGE AHIMIZA WANANCHI KUWA NA UZALENDO, KUJITUMA NA KUJITOLEA KWA MAENDELEO YAO

Na. Ahmad Mmow, Nachingwea.
Mbunge wa jimbo Nachingwea mkoani Lindi, Hassan Masala, amewaasa wananchi wa jimbo hilo kurejesha moyo wa uzalendo kwa kufanya kazi na kuchangia miradi ya maendeleo badala ya kuisubiri serikali.
Hassan Masala
Masala alitoa wito huo juzi katika kijiji cha Nangowe akihitimisha ziara yake ya kuhimiza, kukagua kazi za maendeleo na kuwashukuru wananchi kwa kumchagua.

Mbunge Masala aliwaambia wananchi hawana budi kujitolea katika kujiletea maendeleo yao badala ya kutaka kila kitu kifanywe na serikali.

aliongeza kuwa hakuna serikali yoyote duniani inayoweza kuwachukia wananchi wake wanaoamua kuchangia na kufanya kazi za maendeleo, badala yake itaunga mkono jukudi hizo.
"Changamkieni najitoleeni kuibua miradi ya maendeleo, serikali itawaunga mkono. Msibweteke na kusubiri kila jambo lifanywe na serikali," alisema.

Aidha mbunge huyo ambaye amehitimisha ziara yake ya baada ya kutembelea vijiji 127 vya jimbo hili, alisema zipo kazi ambazo wananchi wanauwezo wa kuzifanya wakati serikali ikiwa inatekeleza miradi mingine ya maendeleo kwa ajili yao.

Alihaidi kushirikiana na wananchi katika kutekeleza miradi watayoibua. Ikiwa ni pamoja na kushiriki kuzifanya kazi hizo kwa kuchangia nguvu na vifaa huku akiisukuma serikali isaidie.

Pamoja na kutoa wito huo, Masala amehaidi kuchangia mifuko 5O ya saruji na bati 50 kwa ajili ya ujenzi wa zahanati ya kijiji hicho.

Kwa upande wake, diwani wa kata ya Nangowe, Ali Chitanda alimueleza na kumuomba mbunge huyo asaidie kuisukuma serikali ipeme viwanja vya makazi katika kijiji hicho. Kwa madai kuwa nyumba wanazoishi zilizopo katika kijiji zimejengwa kwenye maeneo yasiyo pimwa.

Japokuwa kipo jirani na mamlaka ya mji mdogo wa Nachingwea. Kwani ni miongoni mwa kata ambazo zinatarajiwa kuongezwa kwenye mamlaka ya mji mdogo huo ili uweze kuwa Halmashauri ya Mji kamili.
Previous Post Next Post