Hitmaker wa Nyang’anyang’a Shilole,amezidi kugonga vichwa mbalimbali vya habari za burudani tangu kuachana na aliyekuwa mpenzi wake Nuh Mziwanda ambaye pia ni msanii wa Bongo Fleva anaetamba na ngoma yake ya Hadithi.
Moja ya matukio ambayo ameyafanya hivi karibuni ni kutoa maneno machafu baada ya kuulizwa kuhusu kuachana na mpenzi wake Nuh Mziwanda, hali hiyo imejitokeza katika namna nyingine baada ya msanii huyo kualikwa katika kipindi cha Ala za Roho cha Clouds FM kinacho tangazwa na Diva the Bawse.
Katika kipindi hicho Shilole alikwenda akiwa amelewa tilalila jambo ambalo limepelekea kusitishwa kwa kipindi hicho, mwanzo wa kipindi Shilole alianza vizuri ila muda ulivyokuwa unazidi kwenda ndipo hali ilipozidi kubadilika na kuamua kuomba aachwe akalale.
Kitendo hicho cha Shilole kwenda kwenye kipindi akiwa amelewa kilimuudhi mtangazaji Diva na kuhoji inakuwaje mtu unajua unakwenda kwenye mahojiano kisha unakwenda umelewa sana haliyakuwa unajua umuhimu wake.

Katika kipindi hicho Shilole alikwenda akiwa amelewa tilalila jambo ambalo limepelekea kusitishwa kwa kipindi hicho, mwanzo wa kipindi Shilole alianza vizuri ila muda ulivyokuwa unazidi kwenda ndipo hali ilipozidi kubadilika na kuamua kuomba aachwe akalale.

Tags
HABARI ZA WASANII