Unknown Unknown Author
Title: NIMEKUSOGEZEA PICHA KALI ZA WATU WAKIENJOYE CINEMA KWENYE MAENEO TOFAUTI, HUU NI UBUNIFU WA HALI YA JUU
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Kumbe kuenjoy Movie kwenye screen kubwa wewe na watu wako sio lazima iwe kwenye Jumba kubwa la sinema, watu na ubunifu wao wamebuni na h...
Cinema
Kumbe kuenjoy Movie kwenye screen kubwa wewe na watu wako sio lazima iwe kwenye Jumba kubwa la sinema, watu na ubunifu wao wamebuni na hii mtu wangu.. mnaweza kuweka pozi lenu hata kwenye packing ya magari na Movie ikaangaliwa kwa raha zote yani !!
Cinema
Hapa ni Gili Lankanfushi kwenye Visiwa vya Maldives… Hapo ni Hotel ya Kifahari kabisa, mnapewa na nafasi ya kuenjoy movie kwenye eneo la kipekee, pamezungukwa na miti hivi alafu chini ni mchanga kabisa. Kwa wapendanao, YES hapo panawafaa.
Cinema
Hapo panaitwaCinekamari, Visiwa vyaSantorini Ugiriki.Usiogope hivyo vichaka ukahisi Simba au Chui wanaweza kuibuka.. pako salama kabisa na ni sehemu poa pia ya kuenjoy movie na watu wako wa nguvu.
Cinema
Hiyo sio packing ya magari aisee !! Ni Shooting Star RV Resort, Jiji la Escalante, Utah Marekani. Jumanne, Alhamisi na Jumamosi jioni watu wanapaki magari yao, wanacheki movie kwenye Screen kubwa huku wamekaa ndani ya magari yao humohumo.
Cinema
Raha nyingine pembeni ya Bahari, Miami Florida, Marekani.. Minazi, garden poa kabisa ya maua na mapambo mengine vimeongezea uzuri wa hapa, panaitwa Miami Beach Edition Hotel.. unakaa na watu wako mnaenjoy vizuri kabisa movie.
Cinema
Kila mtu na watu wake kwenye bwawa dogodogo, mbele kuna Bonge la Screen ya Movie… Hot Tub Cinema, hizi sehemu ziko Uingereza, Marekani na Ibiza. Unakaa na watu wako kwenye bwawa dogo lenye maji ya moto alafu mnaenjoy movie na story nyingine zinaendelea.
Cinema
Alamo Drafthouse kwenye ubora wake… sahau kidogo kuhusu viti au sofa unapocheki Movie, hapa ni mwendo wa wewe na maji ya Bwawani.. kila mtu na boya lake, mambo yaTexas Marekani mtu wangu..!!
Cinema
Hollywood Forever Cemetary, Los Angeles Marekani.. unaambiwa toka mwaka 2002 watu wa nguvu wamekuwa wakienjoy movie hapo, Bonge la Screen na mazingira poa kabisa kwenye eneo la wazi.
Cinema
Red Rocks Amphitheater, Colorado Marekani.. Jumla ya watu 16,000 wanakaa hapo kucheki Movie mtu wangu.. Hapo ni sehemu ya juu kabisa ya Milima ya Red Rocks Park,kama unakumbuka ngoma ya ‘The Storm Is Over‘ ya staa wa R&B Marekani, R. Kelly alifanyia Video yake hapo juu.
Cinema
Sala Montjuic… Wenyeji wa Canada wanasema ungekuja miaka ya nyuma hapa palikuwa giza tu na pamekaa kihasara bila shughuli yoyote.. sasahivi mida ya jioni watu wa nguvu wanakutana kucheki movie, hakuna kiti !! Kwa hiyo kama ukija na mkeka, godoro au kiti kazi ni kwako !!
Cinema
Soneva Kiri, hapo ni Thailand.. mambo ni kama unavyoona, Screen ya TV iko upande huu alafu watu wanakaa upande wa pili, katikati ni bwawa la maji.. Unaweza ukashtuka kwamba ikitokea El Nino mambo yanakuwaje hapo?? Lakini ndio hivyohivyo watu wa eneo hilo wanaenjoy Movie zaCinema Paradiso.

About Author

Advertisement

 
Top