
Kaimu Katibu Tawala wilaya ya Liwale Ndg: Salum Abdallah Chautundu (Mwenye miwani) akiwa katika Picha ya Pamoja na Kaimu Mkurugenzi Pamoja na Maafisa wa Shirika la Save the Chidren katika kuadhimisha siku ya Unyonyeshaji Duniani ambapo Wilaya ya Liwale imeadhismisha leo Tarehe 10.08.2015 katika viwanja vya Nanjinji.

Kaimu Mganga Mkuu wilaya ya Liwale Ndg Augustino Mchopa Mnape akitoa neno la Shukrani kwa Mgeni rasmi na wananchi waliojitokeza katika Kuhudhuria maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji Duniani ambapo wilaya ya liwale imeadhimisha katika viwanja vya Nanjinjji wilayani humo leo hii tarehe 10.8.2015

Mgeni Rasmi Ndg: Chautundu (mwenye miwani) akiteta jambo na mwenyekiti wa Mtaa Ndg Twahir Mmulila (mwenye tshet Nyekundu) wakati wa Kuzindua wiki ya Unyunyeshazi Duniani ambapo kiwilaya imefanyika Liwale katika viwanja vya Nanjinji. Leo tarehe 10.8.2015
Na.Mwandishi Wetu, Liwale
Kaimu Katibu Tawala wilaya ya Liwale Ndg: Salum Abdallah Chautundu alikuwa Mgeni Rasmi katika Maadhimisho ya Wiki ya Unyonyeshaji Duniani ambayo kiwilaya yamefanyika wilayani Liwale katika Viwanja vya Nanjinji. Maadhimisho hayo yameweza kuhudhuriwa pia na Viongozi wa shirika la Save the Chidren ambao ni wadau wakubwa wa watoto nchini.
Dhumuni la Maadhimisho hayo ni uimarishaji wa lishe kwa wananchi wake ikiwa ni agizo la Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mh. Dkt Jakaya Kikwete. Aidha Kaimu Mganga mkuu wa wilaya ya Liwale Ndg: Augustino Mchopa Mnape alisema kuwa ukiwa na lishe Nzuri basi wewe utakuwa ni mzalishaji mzuri katika sekta yeyoteuliopo hivyo ni dhahiri ya kuwa lishe bora inaanzia kwa mtoto hivyo tunabudi kuhakikisha watoto wetu wanapata maziwa ya mama kwa kipindi husika kwani maziwa ya mama ndio chakula pekee na bora kwa Mtoto ambacho mwenyezi mungu alikitengeneza kwa ajili yake.
Dhumuni la Maadhimisho hayo ni uimarishaji wa lishe kwa wananchi wake ikiwa ni agizo la Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mh. Dkt Jakaya Kikwete. Aidha Kaimu Mganga mkuu wa wilaya ya Liwale Ndg: Augustino Mchopa Mnape alisema kuwa ukiwa na lishe Nzuri basi wewe utakuwa ni mzalishaji mzuri katika sekta yeyoteuliopo hivyo ni dhahiri ya kuwa lishe bora inaanzia kwa mtoto hivyo tunabudi kuhakikisha watoto wetu wanapata maziwa ya mama kwa kipindi husika kwani maziwa ya mama ndio chakula pekee na bora kwa Mtoto ambacho mwenyezi mungu alikitengeneza kwa ajili yake.
Pia aliwasihi wale akina mama weshe fikra potofu kuwa mtoto si lazima anyonyeshwe kwa muda wa miezi sita, alisema Miezi sita ni lazima mtoto anyonyeshwe kama unataka mtoto wako awe mwenye afya nzuri na kipindi hicho ndicho mtoto hujengeka kiakili hivyo usipompa maziwa ya mama hakika unamuweka hatarini katika kushambuliwa na magonjwa na pia kukosa akili za kutosha.
Akisoma Hutuba kwa niaba ya Mgeni rasmi Kaimu Katibu tawala wilaya ya Liwale Ndg: Salum Abdallah Chautundu amewapongeza waandaaji wa Shughuli hiyo kuifanya katika wilaya ya liwale na pia aliwapongeza Shirika la Save the Children kwa kushiriki kikamilifu katika kufanikisha maadhimisho hayo yanafanikiwa.
Aidha mgeni rasmi amesema Hali ya Ugonjwa wa Utapiamlo ipo wilayani mwake ambapo takwimu zinaonyesha ni Asilimia 5 ya watoto chini ya Umri wa miaka 5 wanakabiriwa na ukondefu. asilimia 42 wanatatizo la Udumavu, Asilimia 16 wanauzito pungufu, hivyo kwa takwimu hizo watoto wenye afya njema ni asilimia 37 tu.
Chautundu amesema ilikuwakinga watoto na matatizo hayo ya ukondefu na Utapiamlo ni kuboresha hali ya lishe kwa akina mama wajawazito kabla na baada ya kujifungua. Pia amesema chanzo kingine kinachochangia udhoroteshaji wa afya ni uvunjifu wa haki za uzazi kwa wanawake, hii husababishwa na akina mama kukosa likizo ya uzazi au kipindi cha kupumzika wakati anapokua mjamzito na hata anapokuwa amejifungua hivyo kushindwa kutimiza jukumu la malezi ipasavyo hivyo huchangia hali ya Utapiamlo kwa Mtoto.
Kufuatia Haki ya uzazi kwa Mtumishi sheria ya mwaka 2004, Sheria hiyo inatoa likizo ya siku 84 yenye malipo ya Mshahara kwa wanawake walio ajiriwa na sekta rasmi, aidha endapo mfanyakazi atajifungua watoto mapacha Sheria hiyo inasema atapewa likizo ya siku 100, huku mzazi wa kiume akitakiwa kupewa likizo ya siku 3 ambazo zitatumika kabla ya siku saba baada ya mtoto kuzaliwa.
Aidha sheria hiyo inamruhusu mama huyo baada ya kumaliza likizo yake kupata masaa 2 kila siku kwa ajili ya kumnyonyesha mtoto wake.

Mama mmoja wapo ambaye ananyonyesha akiwa mwenye furaha baada ya Kujibu swali na kupata zawadi ya Kanga kutoka kwa waandaaji wa shughuli ya maadhimisho ya wiki ya Unyonyeshaji Duniani katika Viwanja vya Nanjinji wilayani Liwale leo hii tarehe 10.8.2015

Viongozi wa Shirika la Save the Chidren wakiwa katika Viwanja hivyo kuadhimisha wiki ya Unyonyeshaji Duniani ambapo Kiwilaya yamefanyika wilayani Liwale, leo hii tarehe 10.8.2015

Kikundi cha Ngoma cha UWAKI kikiwaburudisha wakazi wa wilaya ya Liwale walioweza kujitokeza katika viwanja vya Nanjinji kushuhudia maadhimisho ya Wiki ya Unyonyeshaji yaliofanyika leo hii tarehe 10.8.2015 Wilayani humo.
Tags
HABARI ZA KITAIFA