Meneja wa Mfuko wa NHIF Mkoa wa Lindi,Fortunata Kullaya(Alieshika kikombe)Kwa Pomoja na Mkurugenzi wa Masoko, Rehani Athumani (Katikati)na Grace Kisinga Afisa Uhusiano na mawasiliano Nhif wakishangilia Ushindi wa Kwanza Walioupata katika Maonesho ya Nane Nane Kitaifa katika Viwanja vya Ngongo,Manispaa ya Lindi

Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti NHIF akipokea Kikombe cha Ushindi wa Kwanza kundi la Mifuko ya Jamii Toka kwa Rais Jakaya Kikwete,kushoto na Kulia kwa Rais wakishuhudia tukio hilo Ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi,Mwantumu Mahiza na Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika,Stephen Wassira katika Ufungaji wa Maonesho hayo katika Viwanja Vya Ngongo Lindi
Wafanyakazi wa NHIF wakiwa katika picha ya Pamoja katika viwanja vya ngongo lindi
Waziri Mkuu wa Jahuri ya Muungano wa Tanzania,Mizengo Pinda Akisiliza kwa Makini
maelezo ya Huduma zinazotolewa na Mfuko wa Bima ya Afya Toka kwa Mkurugenzi wa
Masoko na Utafiti Bima ya Afya Makao Makuu,Bw Rehani Athuman.Huku Mkuu wa mkoa
wa Lindi na Mtwara wakifuatilia kwa karibu
Jumla ya Wanaume 50 Kutoka maeneo mbalimbali Nchini Wamejitokeza Kupima Saratani ya Matiti katika Banda la Maonesho ya Nanenane la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya -NHIF- Huku Mfuko ukiendeleza Uhamasishaji na uandikishaji wa wajasiliamali katika kujiunga na mpango wa utaratibu wa kupata huduma za matibabu kwa Kadi kupitia vikundi vyao katika sekta zisizo rasmi uliofahamika kwa jina la KIKOA.
Huduma hiyo itakayomsaidia mjasiliamali wa AMCOS,SACCOS,VICOBA na Umoja wa Waendesha Bodaboda na Mama Lishe katika kupata huduma za matibabu pindi anaposhikwa na maradhi kwa kuokoa maisha yake kwa gharama nafuu zaidi katika vituo mbalimbali vya afya.
Katika Maonyesho ya Nanenane Kitaifa yaliyomalizika Mwishoni Mwa Wiki katika Viwanja Vya Ngongo Manispaa ya Lindi ambapo Mfuko wa NHIF ulitwaa kwa Mara Nyingine Ushindi wa Kwanza Katika Kundi la Mifuko ya Jamii Jumla ya wananchi 2000 walijitokeza kupima Afya zao huku wengi wao wakibainika kuwa na Shinikizo la damu huku wakiwa hawajijui
Akiongea na Waandishi wa Habari Mara baada ya kukabidhiwa Kikombe cha Ushindi wa Kwanza na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa NHIF, Bw Rehani Athuman alieleza kuwa changamoto kubwa waliyoibaini katika Maonesho hayo Ni Ukosefu wa Elimu ya Afya
‘Maonesho haya kwa kweli yametusaidia kama Mfuko kwa Kuwa tumeona Uhitaji wa Kutoa Elimu kwa Umma kwa Kuwa Tumebaini Idadi kubwa ya wananchi waliofika baada ya kuwapa Elimu na Kupima wengi walibainika kuwa na Magonjwa bila kujitambua wengine Uzito ukiwa Mkubwa Kuliko Urefu alionao’Alibainisha Rehani
Nae Bi Fortunata Kullaya Meneja wa Mfuko wa Bima ya Afya Mkoa wa Lindi Alisema kuwa Mfuko wake Umejipanga Vema kata Utoaji wa Elimu ya Kata kwa Kata kuhusiana na Umuhimu wa Kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii ili Halmashauri zao ziweze kunufaika na Ruzuku ya tele kwa Tele Ili vituo vya Afya na Zahanati zipunguze makali ya Upatikanaji wa Dawa na Vifaa Tiba
‘Kwa sasa kupitia Elimu iliyotolewa na Mfuko huo tumeweza kupanua wigo katika madawa kwa kufungua maduka madirisha maalum ya dawa kwa wanachama wa NHIF na CHF kwa Kila sehemu ya Huduma za Afya ikiwemo Ufunguzi wa Maduka ya Dawa Muhimu’Alimalizia Kullaya
Mfuko wa Bima ya Afya katika Maonesho hayo ya Nane nane ilitoa Huduma za Upimaji wa Sukari,Saratani ya Matiti, Uzito na Urefu, Shinikizo la Damu na Ushauri wa Afya huku wananchi wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi na Lindi Vijijini wakinufaika na Punguzo la Asilimia 50 Kujiunga na Mfuko wa Afya Ya Jamii (CHF) unaowezesha kaya Kupata Tiba kwa Mwaka baada ya Kujiunga kwa shilingi 5000 kwa wale waliojiunga katika Banda la NHIF
Uhamasishaji kuhusu kujiunga na mpango KIKOA ni muhimu na utamsaidia mjasiliamali kupanga mipango yake ya kifedha bila kuingiliwa na woga wa kupata matibabu pindi anaposhikwa na maradhi Popote Nchini.
Tags
HABARI ZA KITAIFA