Na.Ahmad Mmow,Lindi.
Tatizo la muda mrefu la kivuko kitakachotumika kusafirisha wananchi wa Lindi mjini na kata ya Kitumbikwela, linatarajiwa kumalizika hivi karibuni.
Hayo yalielezwa jana, na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya manispaa ya Lindi, Kelvin Makonda, katika kikao cha baraza la madiwani wa manispaa ya Lindi. Makonda alisema kwakutambua tatizo la muda mrefu la kivuko cha uhakika kitakachotumiwa na wananchi wa Lindi mjini na kata ya Kitumbikwela.
Halmashauri hiyo imenunua boti ya kisasa yenye thamani ya shilingi 50.00 milioni ili kumaliza tatizo hilo. Alisema boti hiyo ambayo inatarajiwa kufika wakati wowote ndani ya mwezi huu itakuwa ni msaada mkubwa kwa shuguli za uchumi na maendeleo kwa wakazi wa kata ya Kitumbikwela yenye vijiji vitano, wa Lindi mjini na maeneo mengine ya jirani."boti hiyo itarahisisha usafiri wananchi wa maeneo hayo hivyo kuchochea na kurahisisha shuguli za maendeleo na kiuchumi kwa wananchi wa pande zote mbili," alisema Makonda.
Alibainisha kuwa hivi sasa wanachi wanaoshi katika maeneo hayo wanatumia muda mwingi ili kuzifikia pande mbili hizo mbili zinazotenganishwa na bahari ya Hindi. Ambapo sasa wananchi wanaosafiri kwa barabara wanatumia saa mbili, lakini boti hiyo itakuwa inatumia dakika saba tu kwa usafiri wa majini. Vilevile mkurugenzi huyo wa manispaa alisema halmashauri hiyo imeweza kuboreshe sekta ya maji kwa wastani wa 198.46 kwa kuongeza visima na vifupi.
Ambapo shilingi 1.5 zimetumika kujenga miundombinu ya maji katika mirad ya Kineng'ene, Tulieni, Mtange, Kitumbikwela, Likotwa na Mingoyo.
"Mahitaji ya maji safi na salama kwa siku ni lita 5518870, lakini maji yanayopatikana ni wastani wa lita 2649057 sawa na 48% ya mahitaji," alisema, Aliyekuwa meya wa manispaa hiyo, Frank Magali. Aliwataka watendaji kuendeleza mshikamano katika kipindi hiki ambacho halmashauri hiyo haitakuwa na wawakilishi wa wananchi.